The House of Favourite Newspapers

Mashine Mpya Imetua Yanga, Yatambulishwa

0

WANANCHI mpooo? Basi kaeni mkao wa kushangilia kwani ile mashine inayojua kucheka na nyavu kutoka DR Congo imetua hapa nchini jana Jumamosi tayari kusaini mkataba wa kuitumikia Yanga.


Mashine hiyo si nyingine bali
ni mshambuliaji, Fiston Mayele aliyekuwa akiitumikia AS Vita ya DR Congo.Mayele alitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar, jana mchana majira ya saa 7:20 kwa ndege ya Shirika la Ethiopia ambapo safari yake ilianzia DR Congo, kisha Addis Ababa, Ethiopia na kituo cha mwisho Dar es Salaam, Tanzania.

Akizungumza na Spoti Xtra baada ya kutua Tanzania, Mayele alisema anajisikia furaha kufika salama, huku akiweka wazi kuwa mara baada ya kusaini mkataba na Yanga, atasalia hapa nchini kwa siku tano kabla ya kurejea DR Congo.

 

“Najisikia furaha kufika Tanzania ambapo nimekuja kusaini mkataba wa kuitumikia Yanga kisha nitakaa hapa kwa siku tano, halafu nitarejea tena Congo kujiandaa ili kurudi kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu ujao.

 

Matumaini yangu ni kufanya vizuri ndani ya Yanga kama ambavyo nilikuambia hapo awali, kikubwa ni kupambana na kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa timu nzima na najisikia vizuri kuwa Yanga kwani nina marafiki kama Mukoko Tonombe, Yacouba Songne na Tuisila Kisinda ambao watanisaidia kufanya vizuri,” alisema mshambuliaji huyo.Rekodi zinaonesha kwamba, msimu wa 2020/21 katika Ligi Kuu ya DR Congo, Mayele alifunga mabao 13 na kutoa asisti nne, huku Ligi ya Mabingwa Afrika akifunga mabao mawili na asisti moja.

MAKAMBO YUPO NJIANI
Wakati Mayele akiwasili nchini
jana, taarifa zinasema kwamba, mshambuliaji, Heritier Makambo raia wa DR Congo, naye yupo njiani kujiunga na Yanga na muda wowote atatua nchini.Makambo ambaye aliwahi kuitumikia Yanga msimu wa 2019/20, hivi karibuni aliachana na Horoya AC na kumfanya kuwa mchezaji huru, huku akiwa tayari amekubaliana kurudi Yanga.

KIUNGO RASTA ASAINI
Wakati huohuo, taarifa
kutoka ndani ya Yanga, zinaeleza kwamba, klabu hiyo imemsainisha kiungo rasta, Hassan Nassor Maulid aliyekuwa akiitumikia Polisi Tanzania.

Leave A Reply