Diamond Kupiga Bilioni 1.78 Marekani

Staa wa muziki barani Afrika, Diamond Platnumz anatarajia kuanza ziara ya kimuziki nchini Marekani ambapo atafanya shoo 11 kuanzia Oktoba 8 hadi 31, mwaka huu.

 

Kwa mujibu wa muandaaji wa shoo hizo, DMK Global Entertainment, sehemu atakazofanya shoo  ni pamoja na Atalanta, Washington DC, Seattle, Minneapolis, Los Angeles, New York, Louisville, Arizona, Boston, Houston na Dallas.

 

Tayari msanii mwingine wa Bongo Fleva, Harmonize naye ametangaza kuanza ziara yake nchini humo kuanzia Agosti 28, mwaka huu ambapo ataanzia katika Jimbo la Ohio.

 

Hivi karibuni, mmoja wa mameneja wa Diamond, Sallam SK, staa huyo anatoza Dola za Kimarekani 70,000 (zaidi ya shilingi milioni 162.2 kwa shoo za nje.

 

Kwa muktadha huo, katika shoo hizo 11, Diamond anaweza kuingiza takriban shilingi bilioni 1.78 ikiwa kila moja atatoza shilingi milioni 162.2 milioni kama alivyoeleza Sallam SK.

STORI NA SIFAEL PAUL | GPL


Toa comment