The House of Favourite Newspapers

Mashtaka 9 Waliyofunguliwa Mahakamani Vigogo 4 wa NEMC

0

Vigogo wanne wa Baraza la Taifa la Hifachi na usimamizi   (NEMC),  wamefikishwa katika Mahakaka ya Hakimu Mkazi Kisutu na wakiiabiliwa na mashtaka tisa likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kutakatisha fedha.

Akiwasomea hati ya mashtaka wakili wa  Serikali, Janeth Magoho amewataja washtakiwa hao kuwa ni Deusdedith Katwale, Magori Matiku, Obadia Ludivick Machupa na Lydia Laurent.

Magoho amewasomea mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Magoho amedai washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kula njama ya kughushi, kutoa nyaraka za uongo, kuisababishia hasara Mamlaka na kutakatisha fedha.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Juni mosi , 2016 na Julai 30, 2017 katika Maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam na Dodoma.

Pia  inadaiwa kati ya Agost 2, 2016 na Septemba 6, 2016 katika Ofisi za Nemc zilizopo Kinondoni, mshtakiwa Katwale alighushi ripoti ya mradi wa ujenzi wa kituo cha mafuta cha Ibra General Enterprise Fuel Filling Station iliyopo kitalu T, kiwanja namba 132 kilichopo eneo la  Chadulu Area A, , jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Katika shtaka la tatu, Katwale anadaiwa kughushi nyaraka akionyesha kuwa kulifanyika mhutasari wa kikao cha kiufundi cha tathimini ya mazingira katika  mradi huo, jambo ambalo sio kweli.

Vile vile  Nyinondi, anadaiwa Julai 5, 2016 katika Ofisi za Nemc wilaya ya Kinondoni, alighushi risiti namba 150784 ya Mei 5, 2016, yenye thamani ya Sh 18.5milioni.

Katika shtaka jingine, Machupa  akiwa katika Ofisi za Nemc Kinondoni, aliwasilisha nyaraka za uongo kwa Yunus Mfala.

Kwa pamoja washtakiwa anadaiwa kuwa wakiwa Watumishi wa Nemc, wanadaiwa kuisababishia hasara baraza hilo, kiasi cha Sh 18.5milioni.

Pia  washtakiwa wanadaiwa kujipatia Sh 18,500,000 kutoka kwa Yunus Mfala , wakati wakijua kuwa Fedha hizo ni zao tangulizi la kughushi.

Hakimu Shaidi, ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 18, 2020 kesi hiyo itakapoitwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa hoja za awali, na upelelezi katika Shauri Hilo umekamilika.

Leave A Reply