The House of Favourite Newspapers

Masikini Dogo Huyu wa Ajax Kama Amekufa Vile

0
Mchezaji wa Ajax, Abdelhak Nouri.

 

SIMANZI imerudi tena kwa wache­zaji, viongozi na mashabiki wa Ajax, baada ya kusikia kuwa mpendwa wao, Abdelhak Nouri, yupo katika hali mbaya na hakuna uwezekano wa kupona.

Kinachowaumiza wengi ni kwamba kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, akiwa na umri mdogo mno, amepata masaibu makubwa yanayomfanya asiwe tena na nafasi ya kufikia ndoto zake.

Familia yake imethibitisha juzi kuwa wameambiwa na madaktari kwamba dogo huyo hawezi kupona.

Dogo huyo alian­guka ghafla uwan­jani baada ya ku­kumbwa na tatizo la moyo akiwa katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na msimu mpya, dhidi ya Werder Bremen wikiendi moja iliyopita.

…Akiwa katika pozi.

Nouri alikim­bizwa haraka hospitali akiwa hajitambui na k u w e k e w a mashine za kumsaidia ku­pumua.

Lakini baada ya kuamka, sasa dogo huyo kwa huzuni nyingi, amepata tatizo kubwa na la ku­dumu la ubongo kutokana na up­ungufu wa oksijeni.

Kwa majonzi makubwa, kaka wa Nouri ameweka wazi kuwa kiungo huyo hataweza tena kutembea, kuzungumza na hataweza pia kuitambua familia yake, huku nafasi ya kupona ikiwa sawa na sifuri.

Hakika maisha hubadilika gha­fla sana kuliko unavyofikiri. Wiki mbili zilizopita hakuna ambaye al­itarajia dogo huyu leo hii atakuwa katika hali hii ya ufu.

Abderrahim, ambaye ni kaka wa Nouri, anasema: “Hataweza kutembea, hatawe­za kuzungumza, hatambui sisi ni akina nani, yaani hatujui kabisa. Hahisi chochote, hasikii chochote.

“Jana (juzi) asubuhi, madaktari walimfanyia vipimo vingine. Eneo kubwa la ubongo limeathirika na halifanyi kazi.

“Kwa mujibu wa madaktari, hata­fanya tena hayo milele, hatapona. Lakini namuamini Allah. Ikiwa hivyo mwisho wa siku nitakubali. Ni kijana mzuri. Kila mtu, dunia nzima, anaon­gea vitu vizuri kuhusu yeye.

“Dini yetu inatu­fundisha kukubaliana na kinachotokea na tunaomba kwa ajili ya uponyaji wake. Mpaka sasa tunashikilia ukweli huo. Hata hivyo, tunaamini kuwa maisha haya ni mafupi na kwamba maisha ya milele yatafua­ta, lakini kila mmoja alitarajia kumuo­na akifunga mabao kwanza.”

Dada wa Nouri, Ghizlan, anaonge­za: “Tunatumaini kwamba siku moja mambo yote yatakuwa mazuri kwa kijana wetu mzuri Nouri.”

Tangu apatwe na masaibu hayo, Nouri ambaye aliibuliwa katika akademi ya Ajax mwaka juzi, amekuwa akipokea sapoti mbalimbali kutoka kwa familia ya soka huku majirani wakiwa wame­piga kabisa kambi nje ya nyumba yake wakiomboleza.

Hata mahasimu wakubwa wa Ajax, PSV Eindhoven, wameonekana kuhusi­ka kutoa faraja katika kipindi hiki kigu­mu huku mastaa wakubwa wa Uholan­zi, Robin van Persie na Georginio Wijnaldum wakiwa tayari wameshatoa sala zao.

AMSTERDAM | CHAMPIONI JUMATANO

 

 

Leave A Reply