The House of Favourite Newspapers

Pluijm Ataka Vifaa Zaidi Singida United

0
Kocha Mkuu wa Singida United, Mholan­zi, Hans van Der Pluijm.

LICHA ya kufanya usajili wa zaidi ya wachezaji tisa wapya, Kocha Mkuu wa Singida United, Mholan­zi, Hans van Der Pluijm, bado hajaridhishwa na usajili huo baa­da ya kuiambia kamati ya usa­jili ya timu hiyo kuwa anahitaji wachezaji wen­gine zaidi.

Mratibu wa kikosi hicho, Festo Sanga, ameliam­bia Championi Jumatatu kuwa Pluijm amewapa majina ya nyota kadhaa kwenye nafasi za kipa na kiungo kwa ajili ya kusajiliwa ili kukiimarisha kikosi chao.

“Tunaendelea na zoezi la usajili, kwani kocha katupa majina ya wache­zaji anaowataka hasa kwenye nafasi za kipa na kiungo mmoja, ambapo mazungumzo na wache­zaji hao ya­naendelea na yakika­milika basi tutawawe­ka hadha­rani kama t u l i v y o ­fanya kwa wachezaji wote tulio­wa s a j i l i , ” alisema.

Leave A Reply