The House of Favourite Newspapers

Masogange Hataki Shobo na Mtu

VIDEO queen matata Bongo aliyeshaini kwenye video mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva, Agness Gerald ‘Masogange’ ameweka wazi kuwa, baada ya kesi yake ya madawa ya kulevya kumalizika, hataki tena kujichanganya na watu kama ilivyokuwa huko nyuma, badala yake anahitaji kutuliza akili.

 

Akizungumza na WIKIENDA, Masogange alisema kuwa, kwa sasa anataka aishi maisha yake ya kawaida na wala hataki kujihusisha na mambo ya kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa mwanzo maana anaona hayo ndiyo yaliyomu-ingiza kwenye misukosuko.

 

“Sasa hivi nataka kuishi maisha yangu ya kawaida kabisa, sitaki tena kujihusisha na mambo ya mitandao, nataka maisha yangu yawe ya kawaida kabisa,” alisema Masogange.

 

Hivi karibuni Masogange alihukumiwa miaka miwili jela au faini ya shilingi milioni moja na nusu baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya.

NA IMELDA MTEMA | IJUMAA WIKIENDA

Comments are closed.