The House of Favourite Newspapers

MASTAA HATARI KWA WANAWAKE

0
Ali Kiba akifanya yake.

KATIKA ulimwengu wa mastaa kuna mambo mengi yanayoendelea yakiwepo mazuri na mabaya pia. Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu lakini ikizidi sana huwa ni kero kwani ndiyo unakuta watoto wa mitaani wanazidi kutokana na wazazi wao kukosa uwezo wa kuwalea au kuachia upande mmoja ulee yaani mwanaume anamwachia mwanamke au mwanamke kumwachia mwanaume. Katika makala hii tunakuletea orodha ya baadhi ya mastaa wa kiume ambao ni mahiri kwa kuwazalisha warembo yaani wanazaa na wanawake tofautitofauti.

BONDI

Msanii wa filamu, Bondi Suleiman ambaye alikuwa ni mwandani wa staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma kabla hawajamwagana hakuwahi kupata mtoto na mwanamama huyo. Lakini Bondi ana watoto watatu kwa wanawake watatu tofauti na hivi karibuni alisema kwamba anafanya jitihada za kuwatafutia maisha mazuri watoto hao ambao wako kwa mama zao na hana mpango kabisa wa kuoa kwa sasa.

Staa wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego.

 

 

MIKE SANGU

Michael Sangu ‘Mike’ ambaye ni msanii wa filamu Bongo alikuwa mume wa ndoa wa msanii mwenzake wa filamu, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ walibahatika kupata mtoto mmoja lakini akawa bahati mbaya kabla ya kutengana. Tofauti na Thea, Mike kwa sasa ana watoto watatu kwa wanawake watatu tofauti na aliwahi kukiri kwamba hana mpango wa kuishi na wanawake hao kwa kuwa waliwahi kuishi waka shindwana hivyo anawalea tu watoto wake wakiwa kwa mama zao hao.

 

ALIKIBA

Staa huyu wa Bongo Fleva anayekimbiza na Wimbo wa Seduce Me ana watoto watatu kwa mama watatu tofauti ambapo amewahi kukiri kwamba mmoja anaishi naye na hao wengine wanaishi kwa mama zao.

 

NAY WA MITEGO

Jina lake halisi ni Emmanuel Elibariki ambaye ni staa wa muziki wa Bongo Fleva ambapo mpaka sasa ana zaidi ya watoto watatu kwa mama tofauti. Amewahi kukiri kuwa na watoto watatu na mama tofauti akiwemo aliyezaa na Siwema, msanii wa filamu, Skaina Ally na wengineo lakini hivi karibuni pia aliibuka mwanamuziki, Faiza Ally na kueleza kuwa amezaa na mwanamuziki huyo hivyo idadi ya awali ikaongezeka.

DUDE Kulwa Kikumba ndiyo jina alilopewa na wazazi wake. Msanii huyu wa filamu licha ya kwamba dini inamruhusu kufunga ndoa nne lakini bado mpaka sasa hajawahi kufunga ndoa licha ya kuwa na watoto saba. Dude ana watoto saba kwa wanawake wanne tofauti ambapo kwa sasa anaishi na mkewe, Eva ambaye amejaliwa kuzaa naye watoto wawili. Tofauti na hao saba pia aliwahi kuibuka mwanamama mmoja na kueleza kwamba amezaa na Dude baada ya kusikia akitaja kuwa ana watoto saba lakini wa kwake ambaye ni ndiyo wa nane hakutajwa lakini msanii huyu amekuwa akiruka kimanga kuhusiana na hilo.

Super Morning: Eneo Alipopigwa Risasi Lissu… Mambo Mapya Tena!

Leave A Reply