The House of Favourite Newspapers

Mastaa hawa safari imewakuta

0

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SIMBA imeamka chini ya Kocha Jackson Mayanja na kufanikiwa kushinda mechi tano mfululizo za Ligi Kuu Bara na kukusanya pointi 15 kibindoni.

Wakati Simba inaamka chini ya kocha huyo Mganda, wachezaji kadhaa wanapaswa kuwa makini, la sivyo safari ya kuondoka Simba itakuwa imewakuta mwishoni mwa msimu.
Mwisho mwa msimu wala si mbali, itakuwa ni Mei 5, mwaka huu na lazima wabadilike, au waikubali safari hiyo.
Ambao wanatakiwa kuhakikisha wanajituma na kubadilika ni Justice Majabvi raia wa Zimbabwe ambaye kiwango chake kimekuwa cha kupanda na kushuka kwa kila mechi, Paul Kiongera, Mkenya ambaye tokea arejee Simba kashindwa kuonyesha ‘maujuzi’ huku majeraha yakimwandama.
Mganda Brian Majegwa, pia lazima achangamke kwa kuwa sasa mara nyingi anatokea benchi kama ilivyo kwa mshambuliaji mkongwe, Mussa Hassan Mgosi. Beki Mohammed Fakhi, naye lazima abadilike, la sivyo, msimu ujao Simba ataiona kwenye ‘kideo’.
Lakini pia kuna wachezaji ambao hata ungemuuliza Mayanja, haraka angewahi na kusema; “abaki”.
Kati ya hao ni Hamisi Kiiza, Mwinyi Kazimoto, Juuko Murshid, Danny Lyanga pia Said Ndemla ambaye ni kijana anayekuwa akionyesha kitu f’lani hivi.
Kinda Hija Ugando pia anatakiwa kubaki kama ilivyo kwa nyota anayeng’ara, Ibrahim Ajib, Abdi Banda, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’. Hata kinda Peter Manyika, naye abaki tu.

Leave A Reply