The House of Favourite Newspapers

Mastaa hawa… ‘wanamiliki mabawa’

0

P-Square-in-private-jet-to-Abijan-Ivory-Coast

Peter na Paul Okoye wakiwa katika ndege yao.

Makala: Boniphace Ngumije

SI jambo la ajabu kumuona staa fulani akimiliki mali zenye thamani kubwa kwa sababu kupitia ‘brand’ ya majina yao pamoja na kazi zilizowapa ustaa huo ni rahisi kutengeneza mtonyo mrefu.
Ndiyo maana halikuwa jambo la kushangaza pale mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon na straika wa Timu ya Antalyaspor ya Uturuki, Samuel Etoo miaka ya hivi karibuni kuonesha hadharani ndege yake binafsi anayomiliki.

Vivyo hivyo kwa Emmanuel Adebayor pamoja na mmoja wa wanawake wanaoongoza kuwa na mtonyo mrefu Nigeria, Folorunsho Alakija ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya kuchimba mafuta ya Famfa. Hawakuishangaza dunia walipoyaanika ‘mabawa’ yao na kuonesha jinsi wanavyoufurahia utajiri wao.
Mbali na mastaa hao na wengine wengi katika tasnia tofauti kumiliki mabawa, katika makala haya wapo mastaa wa muziki kutoka Afrika wanaokula sahani moja na mastaa hao.

 

Akon
Huyu ni staa wa RnB duniani mwenye asili ya Senegal, aliyezaliwa jijini St. Louis, Missouri, Marekani akiitwa Aliaume Damala Badara Akon Thiam. Anamiliki utajiri unaokadiriwa kufikia dola za Kimarekani milioni 300 (zaidi ya bilioni 650).
Akon anaingia kwenye listi hii kama msanii kutoka Afrika kutokana na Jarida la Fobes pamoja na Kituo Kikubwa cha MTV Base kumtaja mara kadhaa kuwa msanii mwenye asili ya Kiafrika mwenye mashabiki wengi zaidi barani kwake. Anamiliki pia taasisi isiyo ya kifaida iitwayo Konfidance Foundation yenye makazi huko kwao Senegal ambapo katika upande wa kujiachia na kuonesha naye ni mmoja wa wasanii waliofanikiwa zaidi duniani, Akon anamiliki ndege binafsi.

P Square
Peter na Paul Okoye ndiyo wasanii wa muziki wanaotajwa kwa sasa kuongoza kwa utajiri Afrika wakimiliki zaidi ya dola za Kimarekani milioni 110 (zaidi ya bilioni 240 za madafu).
Mafanikio yao wameyapata kupitia kazi zao za muziki ambazo ni Personally, Chop My Money, Beautiful Onyinye, Do Me pamoja na Test The Money.
Mbali na mafanikio kupitia nyimbo hizo wakali hao wanamiliki mijengo ya maana nyumbani kwao Nigeria kwenye Kisiwa cha Banana, mingine huko Atlanta, Georgia, Marekani pamoja na ndege binafsi.

Davido-private-jet-1

Davido
“Siku nyingine, dola zingine! Njiani kwenda Togo ndani ya ndege yangu binafsi. Hivi ndivyo inavyokuwa watu wangu!”
Hayo si maneno yangu ni ‘kapsheni’ alizoambatanisha Adeleke David ‘Davido’ kwenye picha alizo ‘share’ na mashabiki wake kupitia akaunti yake ndani ya Mtandao wa Kijamii wa Twitter wakati akiitambulisha ndege yake binafsi miaka ya hivi karibuni.
Alikuwa na umri wa miaka 21 tu wakati ananunua ndege hiyo, kwa sasa Davido ana miaka 23 na ni mmoja wa mastaa wa muziki waliofanikiwa sana Afrika.

Jaguarplane2

Jaguar
Charles Njagua Kanyi ni msanii mwenye mafanikio makubwa Afrika Mashariki akimiliki mali kedekede zenye thamani ya juu ikiwemo mijengo na majumba ya kifahari.
Msanii huyu ambaye ni mshkaji wa karibu wa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na msani kutoka Bongo, Ambwene Yessaya ‘AY’ mwaka 2014 alitua Bongo kwa ajili ya kufanya tamasha akiwa na ndege binafsi anayoimiliki. Hata hivyo, utajiri wa msanii huyu unatajwa kufikia dola za Kimarekani milioni 30 (zaidi ya bilioni 65 za madafu) na kuna uwezekano mkubwa ukaongezeka zaidi kutokana na kuendelea ku miliki miradi mingi.

Leave A Reply