The House of Favourite Newspapers

Mastaa Simba Waonywa na Bodi ya Wakurugenzi Kuhakikisha Hakuna Kupoteza

0

WAKATI Simba SC leo ikitarajiwa kushuka katika Uwanja wa Mkapa, Dar, kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Clube Desportivo 1º de Agosto ya Angola, Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo imeitisha kikao kizito na kuwaonya vilivyo mastaa wake na benchi la ufundi juu ya kuhakikisha hakuna kupoteza nyumbani.

 

Mchezo huo ambao unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni, unakuja baada ya ule wa kwanza uliochezwa Angola wikiendi iliyopita Simba kushinda 1-3 ugenini.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema mapema jana, Bodi ya Wakurugenzi ilifanya kikao kizito na wachezaji pamoja na benchi zima la ufundi, ikiwa ni kuwakumbusha wasione kama kazi imeisha wakati bado.

 

“Maandalizi kuelekeza mchezo wetu kwa ujumla yako vizuri, wachezaji wote wako sawa, hivyo tunaomba tu mashabiki wajitokeze kwa wingi katika mchezo huo ili kukamilisha shughuli yetu pevu tuliyoianza huko Angola.

 

“Mbali na hivyo, kwa kukumbuka historia ya msimu uliopita, Bodi ya Wakurugenzi imefanya kikao kizito na timu nzima kwa maana ya wachezaji na benchi la ufundi, lengo lilikuwa kuwataka wasahau ushindi wa Angola na badala yake waingie mchezoni kwa lengo la kupata ushindi mkubwa ili yasijirudie yaliyotokea mwaka jana.

 

“Tuna uhakika kama wachezaji na makocha watafuata maagizo basi tunaenda kupata ushindi wa mapema, kwani nia yetu ni kuona hatupotezi nyumbani,” alisema Ally.

STORI NA MUSA MATEJA | SPOTI XTRA

KAULI ya ALI KAMWE SUDAN, YANGA IKIJIANDAA KUWAVAA AL HILAL, AOMBA DUA za WATANZANIA..

Leave A Reply