The House of Favourite Newspapers

Mastaa Wa Filamu Bongo Wafurahishwa Na Kuzidi Kunoga Kwa Tuzo Filamu 2023

0
Msanii mkongwe wa filamu za Kibongo, Hashim Kambi.

Dar es Salam 16 Desemba 2023: Msanii mkongwe wa filamu za Kibongo, Hashim Kambi ameelezea kufurahishwa kwake na Bodi ya Filamu nchini chini ya Katibu Mtendaji Dk. Kiagho Kilonzo inavyokuja kasi katika kuendeleza filamu kufikia tamasha la mwaka huu kuvunja rekodi ya ubora na wingi wa viongozi wa serikali.

Katibu Mtendaji Dk. Kiagho Kilonzo akizungumza kwenye tamasha hilo usiku wa kuamkia leo.

Mzee Kambi amesema  hii ni mara ya tatu serikali kupitia Bodi ya Filamu inaandaa tamasha kubwa la tuzo za filamu kama hili, ambapo tulianzia na Mbeya mwaka juzi, mwaka jana lilifanyika Arusha leo ndiyo limefanyika hapa The Super Dome Masaki Dar, lakini kadiri siku zinavyokwenda ndivyo Bodi ya Filamu inavyozidi kuziboresha tuzo hizi na kuzipa thamani kubwa.

JB kushoto na Single Mtambalike a.k.a wakifurahia jambo kwenye hafla hiyo ya utoaji wa tuzo za filamu 2023.

Mzee Kambi amesema kuboreshwa kwa tuzo hizo kumepelekea hata watu wa kuja kushiriki mtuzo hizo na kuzifanya kuwa za kimataifa.

Wasanii wengine wakongwe waliozungumzia ubora wa tuzo za mwaka huu ni Mzee Chilo, Jacob Steven ‘JB’, Madebe Lidai, Mkojani, Gabo, Davina na wengineo.

HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS WA GLOBAL 

FID Q MSIBANI KWA NISHER ASEMA ALIJUTA KUFUNGUA SMS YAKE ALIYOMTUMIA KABLA YA KUFA..

Leave A Reply