The House of Favourite Newspapers

Mastaa Wa Yanga, Max, Skudu Na Nkane Walivyonogesha Uzinduzi wa Maadhimisho Ya Miaka 60 Ya NIC

0
Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Dkt. Elirehema Doriye akizungumza katika uzinduzi wa maadhimisho hayo kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine.

Dar es Salaam 16 Oktoba 2023: Mastaa wa Yanga Max Zengeli, Skudu Makudubela na Denis Nkane kwa niaba ya timu hiyo wameungana na Shirika la Bima la Taifa (NIC) kusherehekea miaka 60 ya shirika hilo ambalo limejivunia kufanya maboresho makubwa ya ubora, uzoefu na udhabiti wa huduma zake kwa jamii.

Katika hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya shirika hilo jijini Dar wachezaji hao walihusika katika matukio mbalimbali ya kuhamasisha kampeni hiyo ikiwemo kukata keki na mengineyo.

Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Dkt. Elirehema Doriye amesema kuwa na wameamua kuitumia Yanga kama rafiki wa kampeni yao ya kusherehekea mafanikio ya miaka 60 ya shirika hilo.

Afisa Mtendaji Mkuu Yanga Andre Mtine (kushoto) wachezaji wa timu hiyo, kutoka kushoto Skudu Makudubela, Denis Nkane na Max Nzengeli kulia wakimpa zawadi ya keki Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Dkt. Elirehema Doriye.

Katika maadhimisho ya miaka 60 ya shirika limekuwa hilo linajivunia manufaa makubwa kutokana na juhudi zinazofanywa na serikali katika kuliinua na kuliendeleza ili kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na bima.

Siku hii ni kubwa sana kwetu kwa sababu tumeona mafanikio makubwa hivyo basi kwa Sasa  tunaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa shirika hili ambapo tunajivunia mafanikio makubwa.

Kwasasa matumaini yetu ni kujiandaa kwa miaka 60 mingine ijayo.

Hafla ya uzinduzi wa maadhimisho hayo ikiendelea.

“Vitu ambavyo tunawekeza kwenye TEHAMA kwa kuwa wabunifu zaidi kwa kubuni huduma ambazo zitabaki kwenye mioyo ya wateja kwani itakuwa kampuni ya kwanza kutumia akili bandia katika utendaji wake.

“Tunaunga mkono vipaumbele vya serikali ikiwemo katika sekta ya kilimo kwa kutoa Bima ya kilimo na pia kufanya shughuli mbalimbali za kijamii katika sekta ya Afya na mazingira.

“Hii ni Bima ya wanachi na tupo kwenye maadhimisho ya miaka 60 lakini pia kuandaa miaka 60 ijayo ambapo tumejidhatiti kutoa elimu kwa wananchi.

Tumejipanga kushirikiana vyema na wananchi katika maadhimisho haya hivyo tutakua na mabonanza mbalimbali ya michezo yatakayohusisha sekta binafsi na serikali wakiwemo waandishi wa habari.” Amesema Doriye.

Kuhusu shirika hilo kutoa bima ya afya Doriye amesema watashirikia na watoa huduma hiyo NHIF ili kuhakikisha wananchi wanapata bima ya afya yenye unafuu na ubora zaidi.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu Yanga, Andre Mtine ameishukuru NIC kwa kuwachagua kuwa nao katika kampeni hiyo na kuahidi kushirikiana nao katika kuhakikisha elimu ya bima inamfikia kila mtu lakini pia kushiriki katika shughuli za kijamii ikiwa kama sehemu ya kutoa elimu.

“Sisi kama Yanga tunashuru kuwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya NIC kwani hii ni taasisi ya kwanza ya bima na inafanya vizuri sana sisi tunaahidi kushirikiana nao.” Alimaliza kusema Mtine. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply