The House of Favourite Newspapers

Mastaa watumika kukamata vigogo wa unga!

0

MASOGANGE5Video Queen, Agness Gerald ‘Masogange’

Stori: Sifael Paul, Ijumaa

Dar es Salaam: Mjini hakukaliki! Mkakati wa Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ wa kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya ‘unga’ hapa nchini, umeiva ambapo uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba unawatumia baadhi ya mastaa Bongo kuwakamata vigogo wanaojihusisha na biashara hiyo.

WAANZIA KWA ‘MATEJA’ Uchunguzi huo wa wiki kadhaa jijini Dar ulibaini kwamba mara tu baada ya Rais Magufuli kutangaza kupambana na mfumo wa wauza unga, kikosi maalum cha Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maofisa wa Uhamiaji waliingia kazini ‘fasta’ ambapo walianza kwa kuwatumia watu wa chini kabisa, kuanzia kwa watumiaji wa unga (mateja) ili kupata mwanga wa wapi wanapopata dawa hizo.

“Kinachofanyika ni kumbana mtumiaji wa unga ‘teja’ ambaye anasema anakopatia unga. Akishamtaja mhusika anayemuuzia, kinachofuata ni kuwaonesha jamaa (polisi na maofisa wa uhamiaji) anakopatikana muuzaji (pusha).
“Wakishamkamata huyo anayewauzia mateja, naye wanambana hadi anawatajia anayempa au kumuuzia hivyo inakuwa rahisi kuwakamata ‘mapapa’ hao wa biashara hiyo iliyokuwa imeota mizizi nchini,” kilinyetisha chanzo chetu ambacho ni mmoja wa watoto wa Kinondoni jijini Dar.

ray-c1 (1)Rehema Chalamila ‘Ray C

WAHAMIA KWA MASTAA
Uchunguzi huo uliendelea kubaini kwamba, wapo baadhi ya mastaa ambao waliwahi kukamatwa, waliohisiwa na wale waliokiri kutumia na baadaye kuacha ambao ndiyo chambo ya kuwanasa wafanyabiashara hao.

MASOGANGE NA MELLISA
“Watu kama Masogange (Video Queen, Agness Gerald) na mwenzake, Melissa (Edward), Julai 2013, walikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini na mabegi sita yaliyobeba dawa za kulevya aina ya Methamphetamine yenye thamani ya Sh. bilioni 7.
“Watu kama hawa ndiyo wanatumika kusema nani aliyewatuma kisha anatiwa mbaroni,” kilidai chanzo hicho.
Katika msala huo, Masogange aliachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, Afrika Kusini baada ya kulipa faini ya Randi 30,000 (zaidi ya Sh. milioni 4.8) huku Mellisa akikutwa hana hatia.

Chid-Beenz_fullChid Benz

MASTAA WENGINE
Mbali na mateja, mastaa mbalimbali ambao walishakiri kutumia dawa hizo na kuacha, nao wamefikiwa na kuulizwa walikokuwa wakizipata dawa hizo ili kufanikisha zoezi la kuwanasa kiulaini vigogo hao.
Baadhi ya mastaa waliowahi kudaiwa kutumia unga na wengine kukiri ni pamoja na Rehema Chalamila ‘Ray C’, Aboubakar Shaban Katwila ‘Q-Chillah’, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ na wengineo ambao kuna madai kuwa nao wamefikiwa ili kujua waliokuwa wakiwauzia unga ili watiwe mbaroni.

WAGOMA KUTAJA WAHUSIKA
Katika mahojiano na Magazeti Pendwa ya Global Publishers, Ray C, Q-Chillah na Chid Benz hawakutaka kuwataja waliokuwa wakiwauzia unga kwa usalama wao na kwamba ishu ni kuacha na kusahau mambo hayo.

WENGINE WALIOHUSISHWA
“Wengine ni wale waliowahi kudaiwa kujihusisha na biashara hiyo kwa sababu ya safari zao za kila kukicha nje ya nchi lakini wakakanusha kama Wanamuziki, Diamond Platnumz (Nasibu Abdul), Jux Vuitton (Juma Khalid), Matonya (Seif Shaban), Bella (Christian Bella) na Shilole (Zuwena Mohamed) ambaye aliwahi kukiri kufuatwa na mtu akimtaka asafirishe unga,” chanzo kiliendelea kumwaga ubuyu na kuongeza:
“Kwa mfano yupo mtu kama Dida (Mtangazaji wa Times FM, Khadija Shaibu), unakumbuka ishu yake ya kuhisiwa mara kwa mara kwa sababu ya safari zake za kwenda China? Kwa vyovyote kwa namna jamaa wanavyonusa lazima watambana tu ili aeleze anachokijua kuhusiana na bishara ya unga.”

MENEJA WA DIAMOND
Wakati wa msala wa Diamond kusafirisha unga, mmoja wa mameneja wake, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ alikanusha vikali akieleza kwamba, utajiri alionao msanii huo ulitokana na shoo nyingi alizokuwa akifanya zilizomuingizia mkwanja mrefu.

UTETEZI WA JUX
Katika kukanusha kwake, Jux yeye alidai kwamba hahusiki kwa namna yoyote na unga na kwamba ishu hiyo ilimuumiza kwani safari zake za China zilihusiana na masomo na biashara nyingine binafsi.

KAULI YA WAZIRI KITWANGA
Kuhusu ishu hiyo, hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga aliwaagiza wakuu wa upelelezi kote nchini kuunda timu za kupambana na dawa za kulevya kwa sababu zinazokamatwa ni nyingi na kwamba hiyo si nguvu ya soda.

“Nimeagiza watendaji wa polisi na uhamiaji pamoja na idara nyingine wanipatie taarifa kila Ijumaa ili watu wanaofanya hizi biashara wafikishwe mahakamani,” alisema Waziri Kitwanga.

Leave A Reply