The House of Favourite Newspapers

Kwa mara ya kwanza ‘Shinda Nyumba’ yatua Mlandizi

0

IKIWA ni mara ya kwanza,  bahati nasibu ya ‘Shinda Nyumba’ inayoendelea kutikisa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar na maeneo mengine ya mikoa ya Tanzania, jana ilionekana kutua Mlandizi Mkoani Pwani ambapo wakazi wa maeneo hayo  walionekana kuvutiwa nayo baada ya kujitokeza kwa wingi kuchangamkia magazeti ya kampuni ya Global Publishers Ltd  kwa kuyanunua na kujaza kuponi ili kushiriki bahati nasibu hiyo.
Mara baada ya maofisa wa Global Publishers, Yohana Mkanda na Jimmy Haroub,  kutua maeneo hayo,  wasomaji wa gazeti la Amani walijitokeza kwa wingi na kununua gazeti hilo kisha kujaza kuponi zinazopatikana kwenye ukurasa wa pili katika gazeti hilo huku pia wakijipatia zawadi za kofia zenye nembo ya Shinda Nyumba zilizokuwa zikitolewa.
Akizungumza na wakazi wa maeneo hayo, Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda, alisema:  “Wanachotakiwa kufanya wakazi wa Mlandizi na maeneo mengine ni kununua magazeti ya Global na kujaza kuponi zinazopatikana ndani ya magazeti  ambayo ni Uwazi, Championi, Risasi Jumatano, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi Jumamosi na Ijumaa ambayo huuzwa kwa sh.  500 na msomaji anaweza kujishindia nyumba ya kisasa.  Kila anayejaza kuponi nyingi anajiongezea nafasi ya kujishindia nyumba na zawadi nyingine,” alisema Mkanda.

1.Muuzaji maarufu wa samaki katika soko la Mlandizi,Soud Kigola(wapili kushoto) akijaza kuponi yake huku wasomaji wengine wa Gazeti la Amani wakimshuhudia.Muuzaji maarufu wa samaki katika soko la Mlandizi, Soud Kigola (wa pili kushoto) akijaza kuponi huku wasomaji wengine wa Gazeti la Amani wakimshuhudia.
2.Bokasa Msuya (watatu kushoto) akijaza kuponi yake huku ofisa Usambazaji Jimmy Haroub (mwenye fulana nyeupe nyuma)akifuatilia wasomaji wa Amani walivyokuwa wakijaza kuponi zao.Bokasa Msuya (wa tatu kushoto) akijaza kuponi yake ambapo Ofisa Usambazaji, Jimmy Haroub (mwenye fulana nyeupe nyuma) akifuatilia zoezi hilo.
3.Wasomaji wa Gazeti la AMani wa eneo la Soko la Mlandizi-Pwani wakichangamkia fursa ya kushiriki Bahati nasibu hiyo ya Shinda Nyumba.Wasomaji wa gazeti la Amani wa eneo la Soko la Mlandizi-Pwani wakichangamkia fursa ya kushiriki bahati nasibu  ya Shinda Nyumba.
4. Mdau maarufu wa Gazeti la Amani anayefanya biashara zake za kuuza duka soko la Malndizi, Andrew Swai akishiriki zoezi la kujaz kuponi ya Shinda Nyumba.Mdau maarufu wa gazeti la Amani anayefanya biashara zake za kuuza duka soko la Malndizi, Andrew Swai, akishiriki zoezi la kujaza kuponi.

5.Mwanadada aitwaye,Selina Damiani (katikati) akijaza kuponi yake ya Bahati nasibu ya Shinda Nyumba mara baada ya kununua Gazeti la Amani kutoka kwa muuzaji wa magazeti,Theresia Julian (kulia).Mwanamama ambaye anafanya biashara zake za kuuza vitambaa katika soko la Mlandizi, Asha Mwakarukwa (kulia) akijaza kuponi yake ya Shinda Nyumba ili kushiriki bahati nasibu hiyo. Anayeshuhudia ni muuzaji wa magazeti ya Global.
7.Mdau wa Gazeti la Amani anayefanya shughuli zake za kuuza vitenge na Khanga katika maeneo ya Mlandizi, Peter P.Marwa akiliangalia gazeti lake ukurasa wa mbele mara baada ya kujaza kuponi yake.Mdau wa gazeti la Amani anayefanya shughuli zake za kuuza vitenge na khanga katika maeneo ya Mlandizi, Peter P. Marwa, akiliangalia gazeti lake ukurasa wa mbele mara baada ya kujaza kuponi yake.
8.Kuponi za Bahati nasibu ya Shinda Nyumba zikiwekwa katika ndoo maalum ya Shinda Nyumba.Kuponi za bahati nasibu ya Shinda Nyumba zikiwekwa katika ndoo maalum ya Shinda Nyumba.
9.Salama Mzuri Salum,mara baada ya kuweka kuponi yake katika ndoo maalum ya bahati nasibu.Salama Mzuri Salum, mara baada ya kuweka kuponi yake katika ndoo maalum ya bahati nasibu.
10.Mwanamama, SalamaSalum (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa muuzaji wa magazeti ya Global,Theresia Julian (kulia) kabla ya kujaza kuponi yake.Mwanamama, Salama Salum (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa muuzaji wa magazeti ya Global, Theresia Julian (kulia) kabla ya kujaza kuponi yake.
11.Wasomaji wakiendelea kujaza kuponi zao.Wasomaji wakiendelea kujaza kuponi zao.
12.Abdallah Hamis (kushoto) akisaidiwa kukata kuponi zake na Ofisa Masoko wa Global,Yohana Mkanda baada ya kujaza kuponi zake.Abdallah Hamis (kushoto) akisaidiwa kukata kuponi zake na Ofisa Masoko wa Global,Yohana Mkanda.
13.Wasomaji wa Gazeti la AMani wakinunua magazeti kwa muuzaji wa Global (katikati) ili kushiriki bahati nasibu hioyo.Wasomaji wa gazeti la Amani wakinunua magazeti kwa muuzaji wa Global (katikati) ili kushiriki bahati nasibu hiyo.
14. Ofisa Masoko wa Global,Yohana Mkanda (kushoto) akishuhudia msomaji wa Amani akijaza kuponi yake. Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda (kushoto) akishuhudia msomaji wa Amani akijaza kuponi yake.
15.Zoezi la kujaza kuponi likiendelea kwa wakazi wa Mlandizi-Pwani.Zoezi la kujaza kuponi likiendelea kwa wakazi wa Mlandizi-Pwani.
16.Shaban Rajab (kushoto) akiweka kuponi zake ili kushiriki bahati nasibu hiyo.Shaban Rajab (kushoto) akiweka kuponi zake ili kushiriki bahati nasibu hiyo.
Na Denis Mtima/Gpl

Leave A Reply