The House of Favourite Newspapers

Mauaji ya Kutisha Dar… Mume Afanya Unyama!

0
Matau Ngosha na Upendo Jonathan, enzi zao.

“KWa kweli ni mauaji ya kutisha! Wakati wakiingia chumbani kwao kulala, hakuna aliyetarajia leo (Ijumaa iliyopita) kama tungeamka na kuambiwa Ngosha na Pendo ni marehemu,” ndivyo walivyokuwa wakisema majirani wa Matau Ngosha na Upendo Jonathan ambao walikuwa mume na mke waliokutwa na umauti usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita.

TWENDE MADALE

Tukio hilo la kutisha lilitokea katika Kijiji cha Nyakasanga, Madale, nje kidogo ya Jiji la Dar ambapo mume, Mat alidaiwa kumuua mkewe kwa kumnyonga chumbani kwao kisha naye alikwenda kujiua kwa kujinyonga kwa shuka kwenye nyumba ya mwalimu iliyokuwa inajengwa.

Ijumaa Wikienda lilifika eneo hilo la tukio muda mfupi baada ya miili ya wawili hao kuondolewa na polisi na kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Lugalo, Dar.

Pendo Jonathan enzi za uhai wake.

DADA WA MAREHEMU ASIMULIA

Akisimulia tukio hilo lililoibua taharuki na simanzi nzito kijijini hapo, dada wa marehemu, Jennifer Mponzi alisema:

“Nilikuwa kazini asubuhi ya leo (Ijumaa), nilipigiwa simu nikaambiwa kuna tatizo limetokea hapa nyumbani, hawakutaka kuniambia ni tatizo gani hadi nilipofika na kukuta mdogo wangu amekufa.

“Nimeumia sana maana mdogo wangu hakuwahi kuniambia kama ana mgogoro na mumewe. Lakini mwanaume anahusishwa na mauaji ya mkewe maana funguo za chumba chao alikuwa nazo mfukoni.

Ndugu wa marehemu.

“Nashindwa kuamini maana jana (Alhamisi) nilipishana na Pendo mjini akiwa kwenye bodaboda na alionekana mwenye furaha kama kawaida.

“Hata jioni majirani waliwaona Pendo na mumewe wakiwa hawana shida yoyote. Kwa hiyo inawezekana ni wivu wa kimapenzi lakini Pendo alikuwa msiri sana maana hajawahi kuniambia chochote kama kuna tatizo.

 

Ndugu wakiwa wameketi.

“Lakini pia kinachoumiza zaidi mtoto wao wa umri wa miaka minne alikutwa ndani akiwa amelala usiku kucha na maiti ya mama yake akidhani mama amelala usingizi wa kawaida, inauma sana jamaniii…!”

 

Ndugu wa marehemu.

MWENYEKITI NYAKASANGA

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mwenyekiti wa Nyakasanga, Peter Bilevera aliliambia Ijumaa Wikienda kwamba, tukio hilo ni mwendelezo wa matukio kama hayo kwenye eneo lake kwani miezi kadhaa iliyopita kijana mmoja naye alidaiwa kujinyonga.

Mwenyekiti wa mtaa.

“Nilipata taarifa, nikafika eneo la tukio, nikatoa taarifa polisi kwenye kituo kidogo cha Madale ambao walifika na kuiondoa miili ya marehemu na kwenda kuihifadhi Lugalo.

“Bado familia zote hazijapanga utaratibu wa mazishi hivyo tunasubiri, lakini ukweli ni kwamba kuna watu wanasema kulikuwa na mambo ya wivu wa kimapenzi,” alisema mwenyekiti huyo.

STORI: GLADNESS MALLYA | NA SIFAEL PAUL, DAR

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Leave A Reply