The House of Favourite Newspapers

Mavugo: Mashabiki Simba Walinipoteza

0

LAUDIT Mavugo ndiyo jina lake lakini Ofi sa Habari wa Simba, Haji Manara alipendelea zaidi kumuita King Laudi.Wakati wa ufalme wa Mavugo, Meddie Kagere hakuwepo hapa nchini.

 

Mavugo aliitumikia Simba kwa muda wa miaka miwili akitokea Vital’O ya Burundi.Turudi nyuma kidogo, Simba walianza kumfukuzia Mavugo mwaka 2015 wakati huo akiwa moto katika Ligi Kuu ya Burundi kufuatia kufunga mabao 32, mwisho wa siku hawakumpata.

 

Harakati za Simba kuendelea kuiwania saini ya mshambuliaji huyo hazikuisha na mwaka 2016 waliipata saini yake.Kabla ya kutua Simba, aliacha rekodi nyingine ya kuwa mfungaji bora tena katika Ligi ya Burundi kwa kufunga mabao 30, hivyo ndani ya misimu miwili akawa ametupia mabao 62.

 

Suala la kufunga kwake lilikuwa jambo jepesi wakati huo lakini mambo yalibadilika na kuanza kumpa wakati mgumu mara alivyoanza kucheza Bongo akiwa na Simba.

Spoti Xtra limefanikiwa kufanya mahojiano na Mavugo anayekipiga katika Klabu ya Napsa Stars ya nchini Zambia na kufunguka mambo mengi juu ya maisha yake ya soka.

 

Mavugo anasema kuwa kwa sasa anamshukuru Mungu kwa kuwa mambo yake yanaenda sawa licha ya kuwa katika majeraha ya kifundo cha mguu yanayoelekea kupona.

 

“Nipo zangu Zambia nimetulia wala sijarudi Burundi kutokana na tatizo la Corona ambalo lipo kila mahali kwa sasa na hata hivyo nilikuwa majeruhi.

 

“Nashukuru nina furaha kuwa hapa, maisha yanakwenda na nimekuwa nikiamini kwamba nitafanikiwa kwa sababu nimekuwa nikijituma ndani ya uwanja kwa kuhakikisha timu inafanya vizuri.

Wakubwa tofauti na Tanzania ambao wengi wanaonekana bado ni vijana.“Nakumbuka mwanzo kwangu ilikuwa shida katika mazoezi kwa sababu mazoezi yao ni magumu halafu ya nguvu tofauti na nilivyokuwa nikifanya wakati nacheza Vital’O na Simba na bila ya hivyo huwezi kufanikiwa kwenye ligi ya hapa.

 

ILIKUWAJE ULIFELI SIMBA?

“Unajua kwanza wakati natoka Burundi nakuja Tanzania kwangu nilikuwa nachukulia kawaida kwamba nakwenda kucheza mpira ambao utaisaidia timu bila ya kuangalia ukubwa wake.“Sasa wakati nafi ka hasa niliposhuka pale uwanja wa ndege kwanza niliona magazeti yana habari yangu na picha kubwa, lakini sijakaa sawa nikaona kundi la mashabiki na viongozi wamekuja kunipokea tena wakiwa na jezi imeandikwa jina langu.

 

“Kiukweli ilinipa wakati mgumu sana kwa sababu Burundi hakukuwa na mambo ya magazeti wala kuona mashabiki wanakufuata vile, presha ilianza kuwa kubwa na nikaona kuna kitu natakiwa kufanya.“Mchezo wangu wa kwanza dhidi ya AFC Leopard katika Simba Day kilichotokea

 

UMECHEZA BURUNDI, TANZANIA NA SASA ZAMBIA, TOFAUTI IPO WAPI?

“Burundi kwanza kuna vipaji vingi vya wachezaji lakini changamoto imekuwa katika ligi kukosa ushindani halafu imekuwa haina malipo mazuri ndiyo maana inakuwa ngumu kuona vipaji vyenyewe.

 

“Lakini kwa Tanzania vipaji vipo halafu ligi yao imekuwa na ushindani mkubwa kuanzia kwa timu hadi kwa mashabiki, lakini hata suala la maslahi kwa Tanzania limekuwa vizuri ndiyo maana wachezaji wengi wamekuwa wakitaka kuja kucheza huko.

 

“Ila hapa Zambia ninachokiona kikubwa cha tofauti na Burundi na Tanzania, hapa ligi yao ni ya nguvu sana, wachezaji wanaocheza ni kilinishangaza kwani mashabiki waliona nimecheza vizuri ingawa kwa upande wangu ilikuwa nimecheza chini ya kiwango.

 

“Nakumbuka baaada ya mechi nilitajwa kila sehemu kuanzia kwenye vyombo vya habari hadi kwa mashabiki na hapo ndiyo nikaanza kupata wakati mgumu kwa sababu presha ilikuwa kubwa kutoka kwa mashabiki.

 

“Binafsi ile hali ya presha ya mashabiki ndiyo nikajiona siyo kitu, natakiwa kuongeza nguvu zaidi nizidi kuonyesha kile ambacho Simba ilikuwa inahitaji lakini kwa bahati mbaya mambo yalikuwa mabaya.

 

“Nilikuwa najaribu kufanya kila kitu kuona nafi kia wanapotaka Simba lakini kila nilivyokuwa nikiingia uwanjani mambo ndiyo yalizidi kuwa mabaya upande wangu, mashabiki wakawa hawanielewi.

 

 

“Nadhani kutokea hapo sikuweza kujua kilichonikuta ingawa walimu kwa upande wao bado waliendelea kuonyesha imani juu yangu lakini bado haikuweza kuwa msaada wa kunifanya kuwa bora,” anasema Mavugo.

 

Mavugo ameanza kuelezea namna presha ya mashabiki ilivyovuruga kipaji chake wakati yupo Simba na kujikuta akishindwa kabisa kutimiza majukumu yake.Usikose sehemu ya pili ya mahojiano haya Jumapili hii ambapo Mavugo ataeleza jinsi alivyowekwa mtu kati na viongozi wa Simba kisa kikiwa ni kiwango chake.Itaendelea…

Leave A Reply