The House of Favourite Newspapers

Mawakili Wasema ‘Puto’ La Seth Limemaliza Muda Wake (Video)

0


MAWAKILI wa bilionea Harbinder Singh Sethi, wameomba daktari maalumu wa mshitakiwa huyo kutoka Afrika Kusini, aweze kuja kumtibia juu ya puto lake kuisha muda kwa madai ya kwamba Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kueleza kuwa hawawezi kufanya upasuaji huo.

Wakili Joseph Sungwa alidai hayo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, wakati shauri hilo linalomkabili Sethi na James Rugemarila lilipopelekwa kwa kutajwa. Sungwa aliwasilisha ombi hilo baada ya Mawakili wa Serikali, Vitalis Peter na Leonard Swai kudai upelelezi haujakamilika haujakamilika na kuomba shauri hilo kuahirishwa hadi tarehe nyingine.

Baada ya Swai kueleza hayo, Wakili Sungwa alidai alielezwa na mteja wake kwamba baada ya kufanyiwa vipimo na Muhimbili, walimweleza hawawezi kufanya upasuaji wa puto. Wakili huyo aliomba daktari wa mshitakiwa huyo wa Afrika Kusini aweze kuja kumtibia au mshitakiwa asafirishwe kupelekwe Afrika Kusini kwa matibabu.

Leave A Reply