The House of Favourite Newspapers

Mawaziri Walivyouaga Mwili Wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Dar Leo

0
Waziri Jenister Mhagama akitoa heshima mbele ya mwili wa Rais Mstaafu Mwinyi.

Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo walikuwa miongoni mwa umati mkubwa uliojitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan ambaye ameagwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

Waziri Angela Kairuki alivyopita kwa simanzi mbele ya jeneza.

Waombolezaji hao walionekana kujawa na simanzi kipindi chote cha tukio hilo ambalo liliongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango ambapo pia alikuwepo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na viongozi wengine.

Waziri Kitila Mkumbo akipita kwa huzuni mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Ali Hassan Mwinyi.                          HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL   
Leave A Reply