The House of Favourite Newspapers

Mayweather Amvaa 50 Cent ‘Unapenda Sana Kiki, Usiniazime Tena Fedha’

MWANAMASUMBWI maarufu duniani wa Marekani, Floyd Mayweather,  ameamua kuamsha bifu na swahiba wake wa zamani, 50 Cent, baada ya rapa huyo kumuandamana Mayweather kwenye mitandao ya kijamii.

Mayweather akitema nyongo kwenye ukurasa wake wa Instagram amefunguka kuwa 50 Cent kwa sasa ana hasira na kila kijana yeyote maarufu na mwenye pesa.  Hii ni kutokana na mpenzi wake wa zamani kukataa kurudiana naye,

Tunajua kwa sasa una hasira sana na kila mtu baada ya mzazi mwenzio wa zamani kukataa kurudiana na wewe, kumbuka yule mtoto uliyezaa naye ni damu yako lakini hujali,“ alisema Mayweather.

Akizungumzia muziki wake kwa sasa Mayweather amesema: “Huna tena ngoma kali (Hit Song) kwenye radio kama tulivyokuzoea miaka ya nyuma, kwa sasa huna hata uwezo wa kuuza ngoma zako kwenye soko, ndiyo maana Interscope (lebo ya muziki) imekupiga chini. Umekuwa mtu wa chuki kwa kila rapa, mwanamichezo na hata wachekeshaji ambao wanaingiza mkwanja mrefu au kufanya vizuri kwa sasa,

Akizungumzia bifu ya 50 Cent na Ja Rule, Mayweather amesema: “Unajifanya unamzonga Ja Rule ili upate kwa kutokea,  ile hali wewe ndiye uliyeiba staili zote za kurap kutoka kwa Ja Rule, ukatuletea staili zako za Ugangster sasa uko wapi? Unaishi kwenye apartment za kimasikini huko New Jersey. nadhani kazi yako kwa sasa ni bora uwe blogger unaweza ukaingiza fedha ila si muziki tena. Eti unanichukia badala ya kujilaumu,  Kanye  West kakumaliza kwenye muziki,“.

Mwanamichezo huyo tajiri zaidi duniani amemuonya pia 50 Cent kuwa asije tena kumuomba au kumuazima fedha huku akimsema kuwa amekuwa mtu wa kupenda vitu vya kiki na umbea kuliko hata kazi yake ya muziki.

Mapema mwezi uliopita 50 Cent alimuita Floyd Mayweather ‘Mtu mjinga zaidi duniani’ baada ya mwanamasumbwi huyo kununua saa yenye gharama kubwa zaidi.

Comments are closed.