The House of Favourite Newspapers

Mazishi ya Patrick: Wema Atangaza Kumaliza Bifu na Muna – Video

STAA wa Bongo Movie, Wema Sepetu amemtaka msanii mwenzake, Rose Alphonce ‘Muna’ kumaliza tofauti waliyokuwa nayo hapo nyuma na badala yake warejshe urafiki wao kama zamani ili waishi kwa upendo na amani.

 

Wema ameyaserma hayo leo Jumamosi, Julai 7, 2018 katika viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni jijini Dar wakatio wa kuaga mwili wa mtoto Muna, Patrick aaliyefariki dunia Nairobi nchini Kenya, Julai 3 na kuzikwa leo katika Makaburi ya Kinondoni.

 

Akiwakilisha wasanii wa Bongo Movies, Wema amesema;

“Pole zangu ziende kwa wazazi wa Patrick ambao ni Muna na Patrick, Muna ni rafiki yangu wa muda mrefu, nisingemjua Muna basi nisingemjua Patrick. Nilimpenda sana Patrick, japo sijabahatika kupata mtoto lakini nafahamu maumivu mnayopitia kwa kupoteza mtoto wenu.

 

“Muna pole sana, najua ulivyompenda Patrick, na mapenzi yako kwake ndiyo yametufanya hata sisi tuwe hapa leo, mimi huwa napenda sana watoto, najua hakuna mzazi anayependa kumzika mwanaye, ninaamini Mwenyezi Mungu atakupa nguvu wewe na baba Patrick.

 

“Ninaomba tuyaache ya mitandaoni, najua mtoto wenu atafurahi huko aliko akiona mnaupendo na hakuna mgawanyiko kama huu ambao tumekuwa tukiuona. Muna unajua nakupenda na nitaendelea kukupenda, yaliyopita si ndwele tugange yajayo,” alisema Wema.

 

Mwaka 2016, Wema aliingia kwenye bifu zito na Muna akiumtuhumu shoga yake huyo kumfanya mama yake ‘ndondocha’ baada ya kuwa karibu na Mama Wema, kumchukua na kumpeleka sehemu za starehe kisha kumlisha maneno ya uchochezi jambop ambalo Wema alichukia na kumfokea vilivyo Muna kupitia akaunti yake ya Instagrm.

VIDEO: WEMA AKIFUNGUKA

Comments are closed.