The House of Favourite Newspapers

MBAPPE ANA BIFU NA KOCHA

STRAIKA yosso wa Paris St. Germain, Kylian Mbappe inasemekana haelewani na kocha wake, Thomas Tuchel na ndio chanzo cha kutoa kauli tata kuhusu mustakabali wake katika klabu hiyo.

Mbappe amechukizwa na kitendo cha Tuchel kutompa nafasi ya kumfanya afunge mabao mengi msimu huu. Dogo huyo aliudhiwa na kitendo cha Tuchel kumweka benchi katika baadhi ya mechi, hali ambayo anaamini imemfanya ashindwe kuwa mfungaji bora barani Ulaya.

Mbappe anaongoza kwa ufungaji kwenye Ligue 1 akiwa na mabao 32 lakini amezidiwa mabao manne na staa wa Barcelona, Lionel Messi, ambaye amekuwa mfungaji bora wa La Liga akiwa amepachika mabao 36. Nyota huyo anaamini kuwa angeweza kumpita Messi kwenye ufungaji bora wa Ulaya msimu huu.


Mbappe, hata hivyo, ameushitua uongozi wa Paris St. Germain baada ya kudai kuwa imefika wakati wake wa kusaka mahali ambako atapewa nafasi ya kuonyesha uwezo katika timu iwe ni PSG au timu nyingine.

“Nadhani imefika wakati kwangu kupata mahali ambako nitapewa nafasi ya kuonyesha uwezo wangu iwe ni PSG itakuwa jambo zuri au sehemu nyingine yoyote nalo litakuwa jambo jema,” alisema Mbappe.


Mbappe anaamini kukosa kwake mechi za dhidi ya Strasbourg au Nantes msimu huu kumechangia kwake kushindwa kumfikia Messi kwa sababu anajiamini angefunga katika mechi hizo.

 

Mbappe amecheza jumla ya mechi 158 na kupachika mabao 90 tangu ameanza soka ya kulipwa mwaka 2015.

PARIS, UFARANSA

 

KOCHA ZAHERA Athibitisha AJIBU Kuchukuliwa na TP MAZEMBE

Comments are closed.