The House of Favourite Newspapers

Mbaroni kwa Kumpa Ujauzito Mwanafunzi

0

POLISI mkoani Morogoro inamshikilia  Samweli Lifa mkazi wa Kilosa (24) kwa tuhuma za kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Mikumi Day iliyopo wilayani Kilosa mwenye umri wa miaka 16.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Fortunatus Musilimu, amesema mtuhumiwa  alitumia mbinu ya kumdanganya mwanafunzi kuwa atamuoa baada ya kumaliza masomo lakini mara baada ya kutimiza lengo lake la kumbaka na kumpa ujauzito alikimbilia kusikojulikana na bado jeshi hilo likamtia nguvuni.

 

Kamanda huyo  ametoa wito kwa jamiii kuacha tabia ya kuwadanganya wanafunzi wa kike kwani jeshi hilo halitawaacha salama.

Leave A Reply