The House of Favourite Newspapers

Mbaroni kwa Kumtumbukiza Mtoto Kwenye Jaba la Maji na Kumuua

0

 

Jeshi la Polisi mkoani Manyara linamshikilia Tluay Shauri (46) mkazi wa kata ya Dareda kwa kosa la kumuiba ndani mtoto wa jirani yake mwenye umri wa miezi mitatu na kumuua kwa kumtumbukiza kwenye Jaba lenye maji wakati mama wa kichanga hicho alipomlaza na kumuacha ndani wakati alipokuwa amekwenda kuchota maji kwaajili ya kufua nguo.

 

 

 

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Paul Kasabago amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtu huyo amekiri kutenda kitendo hicho na tayari ameshakamatwa, huku tukio hiko likihusishwa na ugomvi baina ya familia hizo.

 

 

Kamanda kasabago amesema mtumiwa amekiri kosa akiwa chini ya jeshi polisi na kwamba chanzo cha tukio hilo ni ugomvi baina yake na wazazi wa Kichanga hicho.

 

 

Kufuatia tukio hilo wananchi wakiwemo majirani wa wazazi wa mtoto huyo wameomba hatua kali zichukuliwe kwa muhusika. Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Leave A Reply