The House of Favourite Newspapers

Mbegu za Maboga Zinavyoweza Kukupa Ngozi Nzuri

LEO kwenye safu yetu hii tutaona jinsi mbegu za maboga zinavyoweza kukupa ngozi nzuri na ukawa na muonekano wa kuvutia.

MAHITAJI:

-Kikombe kimoja cha mbegu za maboga.

-Kikombe kimoja cha mafuta ya butter.

-Yai moja.

JINSI YA KUCHANGANYA:

Chukua kikombe cha mbegu za maboga zilizosagwa, changanya na mafuta ya butter yaliyoyeyushwa.

Baada ya hapo lipige yai lichanganye pia ili kuleta urahisi, tumia blenda kusagia mchanganyiko wako ukae vizuri.

Ukimaliza paka mchanganyiko huo usoni acha kwa muda wa dakika kumi mpaka kumi na tano ukauke.

Ukimaliza osha na maji masafi.

Mchanganyiko huu ni mzuri kwa afya ya ngozi lakini pia husaidia kuondoa uchafu wote pamoja na chunusi ndogondogo

Na Hamida Hassan

Comments are closed.