The House of Favourite Newspapers

Mbele ya Waziri Mkuu NMB Yajipanga Kusaidia Kufufuliwa Zao la Mkonge

0
Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao mkonge uliofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jijini Tanga.

Benki ya NMB imesema kuwa itahakikisha inaendelea kutoa huduma za kifedha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kufufua zao la Mkonge na kuboresha uchumi wa wakulima wa zao hilo nchini. Hatua hiyo inakuja baada ya serikali kuanza mikakati ya kuhakikisha zao hilo linafufuliwa na kuwanufaisha wakulima na taifa kwa ujumla kama ambvyo ilivyokuwa miaka ya nyuma.

 

Akiongea mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa kikao cha wadau wa Mkonge kilichofanyika jana Mkoani Tanga, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki hiyo – Filbert Mponzi, alisema kuwa NMB itaendeleza jitihada za kufufua zao hilo ambazo imezianza.

Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao mkonge uliofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jijini Tanga.

Alisema kuwa tangu serikali imeanza kulifufua zao hilo Benki hiyo imekuwa ikitoa ushirikiano ambapo imetoa zaidi
ya Bilioni 1 kwa ajili ya ununuzi wa matrekta 11 na trela 22 vifaa ambavyo vitapunguza gharama ya uendeshaji na
kuongeza tija na pato la wakulima wadogo wa mkonge.

 

Aidha aliongeza kuwa Benki hiyo imeendelea kutoa mikopo ya pembejeo na uendelezaji wa mashamba ya Mkonge
kwa wakulima wadogo, kati na wakubwa ili kuongeza uzalishaji na mapato ambapo zaidi ya shilingi bilioni 6
zimeshatolewa kwa wakulima wa mkonge.

Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Horticultural Association (TAHA), Jaqueline Mkindi wakati wa mkutano wa wadau wa zao mkonge uliofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  jijini Tanga.

Alisema kuwa NMB imefanikisha kufungua akaunti kwa wakulima zaidi ya 1,500 ambapo akaunti hizo zinajumuisha
wakulima mmoja mmoja na wale wanaozalisha kupitia Vyama vya Msingi.
“Uwepo wa akaunti hizi unajenga utamaduni wa wakulima kutumia huduma za benki kwa usalama wa fedha
zao na mazingira sahihi katika kupata huduma zaidi ya kifedha ikiwemo Mikopo” alisema Mponzi.

 

Mheshimiwa Waziri Mkuu ili kuendelea kuwajengea uwezo wakulima wadogo na kupata mitaji NMB kupitia
taasisi kanzu ya NMB Foundation inaendelea kutoa mafunzo kwa wakulima kupitia vyama vya vya msingi na
kikundi ili kuimarisha utendaji na kuongeza soko," alifafanua.

 

Mponzi alibainisha kuwa Benki ya NMB itaendeleza jitihada hizo, ikiwemo kutoa mikopo mikubwa, midogo na ya
kati ili kuhakikisha wakulima wa zao wanazlisha kwa tija.
“NMB tutaendelea mikopo katika ngazi zote za uzalishaji wa zao la mkonge, ikijumuisha mikopo ya muda mfupi
na muda wa kati (yaani uwekezaji). Mikopo hii inajumisha pembejeo, upanuzi na miundo mbinu ya mashamba,
matrekta, mashine za uchakataji wa mkonge, viwanda vya mkonge pamoja na huduma mbalimbali katika
sekta,” alisema.

Akizungumza katika kikao hicho cha wadau wa zao la Mkonge, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa mpaka
kufikia mwaka 2025 Tanzania inatarajia kuzalisha tani 120,000 za Mkonge kwa mwaka. Majaliwa alisema kuwa zao
la Mkonge ni miongoni mwa mazao ya biashara hapa nchini ambayo mikakati yake ilitekelezwa vizuri itawezesha
serikali kupata fedha za kigeni lakini pia kukuza pato la mwananchi mmoja mmoja.

 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alisema kuwa kwa sasa Wizara tayari imeshatenga shilingi
Bilioni 175 kwa ajili ya kufanya utafiti ili kuzalisha mbegu bora na zenye gharama nafuu.
Bashe alisema kuwa Wizara imeweza kuandaa utaratibu wa hati ya dhamana (LC) utakaowezesha wakulima
wadogo kuchukua mkopo kwenye taasisi za fedha kwa riba ya asilimia mbili tu.

Leave A Reply