The House of Favourite Newspapers

Mbeya, Kilimanjaro Waongoza kwa Wanawake Wenye Vitambi

0

WANAWAKE wa Mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya na Arusha wanaongoza kwa kuwa na unene uliopitiliza na kupata viribatumbo maarufu kitambi.

 

Akizungumzia kilele cha maadhimisho ya Siku ya Lishe kitaifa, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Dk Germana Leyna amesema utafiti uliofanywa katika mikoa hiyo inaonyesha Kilimanjaro inaongoza kwa kuwa na asilimia 49 huku Arusha na Mbeya zikishika nafasi ya pili kwa kuwa na asilimia 30.

 

Dk Leyna alisema utafiti huo umefanywa kwa wanawake walio katika umri wa kuzaaa kuanzia miaka 15 mpaka 49.

 

“Sababu kubwa ni kula kupita kiasi cha kawaida hasa wazazi wanaotoka kujifungua , mabadiliko ya uandaaji wa vyakula, mfuno wa maisha lakini pia kuweka mkazo katika vita dhidi ya utapiamlo jambo lililochagia watu kula zaidi bila kuzingatia kanuni za ulaji.”

Leave A Reply