The House of Favourite Newspapers

Mbeya: Waziri Mkuu Atoa Siku 2 Madiwani Wamalize Tofauti Zao

0
Kassim Majaliwa.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewapa siku mbili Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya kumaliza tofauti zao zinazokwamisha utendaji wa Halmashauri hiyo na kuendelea kufanya kazi walizotumwa na wananchi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo Kyela Mbeya baada ya madiwani hao kuwa na tofauti kwa takribani mwaka mmoja jambo ambalo linapelekea viongozi hao kushindwa kufanya maendeleo katika halmashauri hiyo.

Majaliwa amedai ikifika Jumatatu (Julai, 31, 2017) Madiwani hao wawe wamemaliza tofauti zao na wawaite wakuu wa Idara na kuwapa taarifa hiyo ili shughuli za maendeleo ziendelee kutekelezwa ndani ya Halmashauri hiyo.

“Baraza la Madiwani limegawanyika mna mgogoro tunataka uishe na mshirikiane na mshikamane katika kufanya shughuli za maendeleo ili wananchi waweze kupata manufaa. Mkiendeleza migongano hatutawavumilia, Serikali inauwezo wa kulivunja baraza. Naombeni mmalize tofauti zenu mara moja kabla sijaondoka.” alisema Waziri Mkuu.

 

Waziri Mkuu amesema madiwani hao wamekuwa na mvutano kati yao kutokana na baadhi ya madiwani hao kuwatetea watumishi ambao wamesimamishwa kazi kutokana na ubadhilifu na kuiba fedha za serikali zaidi ya mabilioni.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameiagiza Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mbeya kuhakikisha watumishi wote waliohusika katika kula fedha za umma wanachukuliwa hatua kama alivyopendekeza Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).

Chanzo: EATV

Leave A Reply