The House of Favourite Newspapers

Mbezi, Kiluvya na Kibaha… Gazeti Jipya la Ijumaa ndiyo habari ya mjini

0

SAMSUNG CAMERA PICTURESHasani Issa  wa kiluvya akinunua gazeti la Ijumaa kwa Tsh. 1000/= kutoka kwa muuzaji magazti ya Global Publishers, Khadija Rashid jana, Julai 15.

SAMSUNG CAMERA PICTURESMama Khalid wa Kiluvya, Dar akisoma gazti la Ijumaa, jana, Julai 15..

SAMSUNG CAMERA PICTURES

Mkazi wa Kibaha-Picha ya Ndege akisoma strori zilizomo kwenye gazeti la Ijumaa.

SAMSUNG CAMERA PICTURESMkazi wa Kibaha Bi. Magreth akiwa na nakala yake ya gazeti la Ijumaa baada ya kununua.

SAMSUNG CAMERA PICTURESSuleiman Ramadhani wa Kibaha akisoma gazeti la Ijumaa toleo la Julai 15.

WASOMAJI mbalimbali wa maeneo ya Mbezi, Kiluvya na Kibaha jana walizidi kufurahishwa na muonekano mpya wa gazeti la Ijumaa baada ya kulichangamkia wakati gari la matangazo lilipokuwa likipita mitaani.

Akizungumza na wakazi wa maeneo hayo, Ofisa Masoko wa Global Publishers inachapisha gazeti hilo pamoja na yale ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani na Championi, Yohana Mkanda, aliwataka kuendelea kulinunua gazeti hilo pekee linalouzwa shilingi elfu moja miongoni mwa yote ya Global, ili waweze kupata habari na uhondo mwingine kama burudani, hadithi, machombezo na mikasa.

“Magazeti mengine ya Global yanauzwa kwa shilingi 500 isipokuwa Ijumaa pekee lenye muonekano mpya ndilo linauzwa shilingi 1000. Niwasihi wasomaji wetu waendelee kununua magazeti yetu ili wazidi kuhabarika, kuelimika na kuburudika,” alisema Mkanda.

NA HIRALY DAUDI/GPL

Leave A Reply