The House of Favourite Newspapers

Mbio za Mwenge wa Uhuru Zakwama Morogoro Kutokana na Mafuriko

0

Mwenge wa Uhuru unaoendelea na mbio zake mkoani Morogoro, umekwama kwa saa kadhaa baada ya Mto Lulai uliopo katika Kijiji cha Kidugalo Kata ya Ilagua wilayani Ulanga mkoani humo kufurika maji na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara ya Rupiro- Malinyi.

Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Salim Alaudin Hasham amesema changamoto ya Mauriko katika wilaya ya hiyo imeathiri maeneo mengi ambapo zaidi ya kaya 400 zimekosa makazi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Dokta Julius Ningu amesema tayari changamoto hiyo imeripotiwa kwenye mamlaka husika lli iweze kutatuliwa na mwenge kuendelea na mbio zake.

Leave A Reply