The House of Favourite Newspapers

Mbongo Afunika Mbaya Bundesliga

MDENMARK Yussuf Poulsen, ambaye mama yake ni mtanzania alifunika kwenye Bundesliga baada ya kupiga mabao mawili na kutoa asisti moja wakati timu yake ya RB Leipzig ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bayer Leverkuse, wikiendi iliyopita.

 

Ushindi huo uliisaidia RB Leipzig kuchupa hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Bundesliga. Poulsen, ambaye baba yake ana asili ya Denmark, alipachika mabao yake katika dakika za 27 na 85 wakati pia akitengenza bao jingine lililopachikwa na Klostermann katika dakika ya 67.

Mabao hayo yamemfanya staa huyo kufi kisha mabao sita ya Bundesliga. Poulsen, ambaye amecheza mechi 29 za Bundesliga tangu msimu wa 2016/17, alipongeza umahiri wa timu yake katika kucheza soka la kushambulia na kujihami.

 

Leipzig haijapoteza mechi ya Bundesliga tangu ilipofungwa na Borussia Dortmund kwenye mechi ya kwanza ya msimu huu. Pia timu hiyo kwa mara ya tano mfululizo haijarahusu bao katika nyavu zake.

LEIPZIG, Ujerumani.

NOW AM HERE: MWIJAKU – “Bwana wa MOBETO ni TAPELI, kapotea njia”

Comments are closed.