The House of Favourite Newspapers

Young Thug Aachiwa na Mahakama, Apewa Masharti – VIDEO)

BAADA ya rapa Young Thug kuwekwa ndani kwa siku sita kwa kosa la kutumia madawa ya kulevya, hatimaye mahakama imemwachia huru ila kwa masharti maalumu.

Mahakama imeamua msanii huyo  arudi nyumbani lakini anatakiwa kupeleka vipimo vya matumizi ya madawa ya kulevya japo mara mbili kwa wiki huku pia akizingatia ushauri na kuonana na msimamizi wake wa uangalizi.

Novemba  14 mwaka huu, rapa huyo aliripoti makahamani na kuomba msamaha na kusema:

“Samahani kwa kutotii amri ya mahakama ,nahitaji kwenda nyumbani kwa familia yangu na kufanya mema, kwa muda wa siku sita nimeelewa maisha. Nina watoto wawili, mmoja ana miaka kumi, mwingine kumi na moja, sipendi waone kwamba nakwenda jela, nataka kukua na nataka wakue.  Nimefanya makosa na ninaomba msamaha, sitakiuka tena amri ya mahakama.”

Mnamo 2017, rapa huyo alikumbwa na kesi baada ya kupatikana na madawa ya kulevya aina ya Hydrocodine, Generic Xanax, Codein, Bangi, Dola 50,000 taslim, na silaha ambayo haijasajiliwa ndani ya gari aina ya Mercedes-Benz Maybach.

TAZAMA VIDEO AKIOMBA RADHI

Comments are closed.