The House of Favourite Newspapers

Mboso: Krismasi Hii Dar Live Patakuwa Hapatoshi

0

MKALI anayekimbiza kunako Bongo Flevani akitokea Usafini, Mbwana Yusuf Kilungi ‘Mbosso Khan’, ameapa kufanya balaa siku Krismasi Desemba 25, ndani ya Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar.

 

Mbosso ameiambia Mikito Nusunusu kuwa, siku hiyo atapiga shoo baab’kubwa kwani ni muda mrefu umepita hajafanya shoo Mbagala na ana hamu sana ya kufanya shoo huko kwani ndiko nyumbani kwao.

 

“Aah kwanza niseme tu nimejipanga vizuri kabisa bila kipingamizi nina mazoezi ya kutosha kabisa hivyo watu wangu wa Mbagala wategemee kitu kikubwa na naahidi sitawaangusha.

 

“Siku hiyo kwanza watajua kama kweli naitwa Mbosso kwani nimewaandalia madude ya kutosha ambayo naamini watayafurahia vya kutosha, hapa ninavyoongea na wewe nimetoka kumaliza mazoezi na madansa wangu na wao wameahidi kitu kizuri tu, Mbagala wakae mkao wa kula,” alisema Mbosso.

STORI: Ammar Masimba

Leave A Reply