The House of Favourite Newspapers

Mbowe Afunga Mjadala wa Lowassa, Amtaja Dkt. Slaa!

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema uamuzi uliofanywa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa wa kukihama chama hicho yalikuwa ni maamuzi yake binafsi.

 

Freeman Mbowe ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya siasa nchini ambapo kwa sasa amesema amefunga mjadala wa kiongozi huyo.

 

Mbowe amesema:“Kuhusu aliyekuwa mgombea wetu 2015, Edward Lowassa baada ya kurudi CCM, vyama vyote vinakusanya watu kwa mahitaji maalumu na watu hao wanakuwa na mambo yao pengine kutaka kuwatumikia watu au tamaa ya madaraka.

 

“Vyama vya siasa ni dodoki, wapo tulioanza nao hawakuwa Edward Lowassa, wakaondoka, wapo waliojiunga na chama katikati wakaondoka, kila mmoja wetu ana utashi wake, ana hulka zake.

 

“Kuhusu Lowassa nilishasema na nikafunga mjadala, tumepokea viongozi wengi siyo Lowassa peke yake, tulimpokea Dkt Slaa alitoka CCM, mwaka 1995 aliwania ubunge wa Karatu kwa tiketi ya CCM, akakatwa kwenye kura za maoni, wazee wakamleta Chadema, tumekaa naye miaka mitano alikuwa bado akivaa mashati ya CCM.”

 

Kuhusiana na kukaa magerezani kwa muda mrefu Mbowe amesema: “Kuna ugonjwa uliopo magereza kwa lugha ya huko unaitwa ‘Burudani’ ambao ni ugonjwa wa ngozi na unaambukiza, chanzo chake ni kunguni na chawa”.

 

Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wamekaa kwa zaidi ya miezi mitatu gerezani kutokana na kosa la kukiuka masharti ya dhamana.

Comments are closed.