Kupitia kwao, Mheshimiwa Mbowe amewataka Wakenya wote kushikamana kuhakikisha kuwa uchaguzi
wao unakuwa wa haki, huru na wazi.
Kipekee, amewasihi Viongozi na Wagombea hao kuhakikisha vurugu za uchaguzi zilizotokea nchini Kenya miaka ya nyuma na kusababisha vifo vya Wakenya kamwe havijirudii tena.
Aidha, amewataka kutambua nafasi ya Taifa la Kenya katika kuendeleza Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu katika Eneo la Jumuia ya Afrika Mashariki na kwamba wanapaswa wakati wote kulinda na kuendeleza mafanikio hayo.
Mheshimiwa Mbowe amewatakia Wakenya wote mchakato mwema wa Uchaguzi wao wa August 2022.