The House of Favourite Newspapers

Mbowe Ataka Kesi Yake Isiendeshwe na Mahakama ya Mafisadi

0

MAWAKILI wa upande wa Utetezi Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wakiongozwa na Peter Kibatala wameitaka mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi (Mahakama ya Mafisadi) kuwaachia huru Mbowe na wenzake kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za ugaidi.

 

Mahakama hiyo imesema kuwa itatoa uamuzi huo kesho Jumatano, Septemba 1, 2021 kama inayo mamlaka ama haina mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi hiyo.

Mbowe na wenzake wameipinga mahakama hiyo kuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi yao kwa mashtaka ya ugaidi na kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia Ugaidi kesi yao inapaswa kusikilizwa na Mahakama Kuu ya kawaida na si hiyo ambayo ni Divisheni Maalum.

Upande wa Serikali umepinga hoja hizo ikidai kuwa kwa mujibu wa marekebisho ya sheria mbalimbali namba 3 ya Mwaka 2016 makosa yaliyoko kwenye Sheria ya Ugaidi yaliwekwa kwenye Sheria ya Uhujumu Uchumi na kwamba kwa hali hiyo mahakama hiyo ya ufisadi ina mamlaka ya kusikiliza mashtaka yao.

Jaji Elinazer Luvanda baada ya kusikiliza hoja za pande zote ameahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumatano asubuhi atakapotoa uamuzi.

Leave A Reply