The House of Favourite Newspapers

Mbowe Mgonjwa, Ashindwa Kufika Mahakamani – VIDEO

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, leo Alhamisi, Januari 17, 2018 ameshindwa kabisa kufika katika Mahakama ya Kisutu kwa sababu zilizoelezwa kuwa ni mgonjwa.

 

Wakili wa Serikali mwandamizi, Patrick Mwita ameeleza hayo, mbele ya hakimu mkazi mkuu, Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa ambapo amedai kuwa shauri hilo wanasubiri maamuzi kutoka Mahakama ya Rufani huku Hakimu Mashauri akiahirisha kesi hiyo hadi, Januari 31, mwaka huu.

 

Mbowe na Mbunge mwenzake, Ester Matiko, wanaendelea kusota rumande kutokana na kufutiwa dhamana baada ya kukiuka masharti ya dhamana yao.

 

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya jinai namba 112/ 2018 ni Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya, Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.

 

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16 mwaka huu maeneo ya Dar es Salaam.

 

Comments are closed.