The House of Favourite Newspapers

Mbrazil Simba SC Aanguka Mazoezini, Ashindwa Kuona

KATIKA hali ya kushangaza jana beki wa kati wa Simba, Tairone Santos raia wa Brazil alianguka ghafla kutokana na kupatwa na kizunguzungu.

 

Beki hiyo alianguka wakiwa akiwa kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar hali iliyosababisha kulipa wakati mgumu jopo la madaktari wa timu hiyo wakiongozwa na Yasini Gembe kutokana na kushindwa kuelewana lugha.

Championi Jumamosi ambalo lilikuwepo kwenye mazoezi hayo, lilimshuhudia beki huyo wa kati akishindwa kuendelea na mazoezi baada ya kujiweka pembeni kabla ya kulala chini kutokana na kushindwa kuona baada ya kukumbwa na kizunguzungu.

 

Baada ya kuanguka, Gembe alimkimbilia na kuanza kumpa huduma ya kwanza kisha baadaye Mtaalam wa Tiba na Lishe, Paul Gomes kuungana naye lakini hawakuweza kutambua kwa haraka.

 

Beki huyo aliendelea kulala chini mpaka kiungo mwingine Mbrazil, Gerson Fraga kuitwa eneo la tukio kwa ajili ya kuwasaidia kwenye mawasiliano ambapo walijua tatizo lake.

 

Baadaye Tairone aliondolewa uwanjani hapo akiwa ameshikiliwa kwa kuwa hakuwa anaona chochote. Championi lilimzungumza na Daktari wa timu hiyo, Yasin Gembe ambaye alisema kuwa:

 

“Kilichotokea kwa Tairone siyo jambo kubwa au la kushtua ila ni hali ya hewa kwa sababu kulitoka jua kali sana ambalo lilikuwa linaumiza ndiyo lilisababisha apate tatizo la kushindwa kuona huku akikumbwa na kizunguzungu lakini kwa sasa anaendelea vizuri.”

Comments are closed.