The House of Favourite Newspapers

Mbunge Ataka Jaji Mkuu Aondolewe kwa Kufuta Uchaguzi wa Rais

0
David Maraga (kushoto) na Mbunge Ngunjiri Wambugu

MBUNGE wa umoja wa kisiasa wa Jubilee nchini Kenya amewasilisha muswada bungeni akiitaka Mahakama Kuu nchini humo kumwondoa madarakani Jaji Mkuu, David Maraga, aliyefuta matokeo ya uchaguzi wa urais nchini humo.

Mbunge huyo, wa Nyeri, Ngunjiri Wambugu, ameitaka Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) kumwondoa jaji huyo kwa kufuata matokeo ya uchaguzi ambao Rais Kenyatta anadai alishinda.

Akizungumza nje ya Mahakama Kuu, Wambugu alisema Maraga aliwashawishi majaji wenzake kufuta matokeo hayo na kwamba uamuzi huo ulihusisha majaji ambao wana uhasama na Jubilee.

Majaji wa Mahakama Kuu Kenya.

Kutokana na uamuzi huo tume ya uchaguzi nchini humo imepanga Oktoba 17 kuwa siku ya kurudiwa uchaguzi wa rais nchini humo ambapo umoja wa vyama vya upinzani ujulikanao kama NASA umetishia kususia iwapo tume hiyo (IEBC) haitabadilishwa, ikiwa ni pamoja na kumwondoa ofisa wake mkuu, Ezra Chiloba.

Septemba 1 mwaka huu Mahakama Kuu nchini Kenya ilifuta matokeo ya kuchaguliwa tena kwa Rais Uhuru Kenyatta ikisema tume haikufuata matakwa ya katiba kuhusu uchaguzi nchini humo. Majaji wanne, akiwemo Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu Justice Philomena Mwili, Smoking Wanjala na Isaac Lenaola waliyafuta matokeo ya uchaguzi huo.

Hata hivyo, Jaji Njoki Ndung’u na Ojwang hawakukubaliana na uamuzi huo ambapo Jaji Ibrahim hakutoa maoni yake kwani alikuwa mgonjwa. Baada ya kufutwa kwa matokeo hayo, Rais Kenyatta aliwashambulia majaji hao akiwaita “wakora” yaani wahuni. Aliwaita hivyo katika mkutano wa hadhara mjini Kisii.

Shuhudia Yusuf Manji Alivyoachiwa Huru na Mahakama ya Kisutu

Leave A Reply