The House of Favourite Newspapers

Mbunge Ataka Serikali Ianzishe Chuo cha WIZI – Video

0

BUNGE la Bajeti, mkutano wa 19 kikao cha 38 limeendelea kujadili hoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa [LAAC] kuhusu ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali [CAG] huku serikali ikishauriwa kuanzisha Chuo cha Wizi ili kukabiliana na ubadhirifu wa mali za umma.

 

Wakitoa michango ya maoni mbalimbali jana Mei 28, 2020 juu ya Ripoti ya CAG iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa [LAAC], Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba, ameshauri serikali kuanzisha chuo cha wizi ili kuweza kupambana na ubadhirifu wa mali za umma.

 

Naye Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi,  amesema kuna baadhi ya watumishi ngazi ya halmashauri wasiokuwa waaminifu wamekuwa wakitumia mashine za ukusanyaji mapato [POS] kwa njia ya udanganyifu na kusababisha halmashauri kupata hasara hivyo kuna haja ya kuwafukuza.

 

Vilevile, Naibu Waziri wa Kazi ,Ajira na wenye Ulemavu, Stella Alex Ikupa, amesema serikali ya awamu ya tano imekuwa na mchango mkubwa katika kuwezesha mikopo watu wenye ulemavu, ambapo Naibu aziri Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.Mary Mwanjelwa ametoa pongezi kwa watumishi kwa kufanya kazi bila kuchoka.

 

Pia Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Agelina Mabula, amesema wizara hiyo imesogeza huduma za ardhi ngazi ya mikoa huku Naibu Waziri wa ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa akizungumzia suala la mapato zaidi ya bilioni 17 ambazo hazikwenda kwenye miradi ya maendeleo.

 

Kuhusu posho ya madiwani, Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa [TAMISEMI] Seleman Jafo, amesema kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, zaidi ya sh. bilioni 10 zimeshalipwa huku Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa [LAAC] Vedasto Edgar Ngombale, akihitimisha hoja ya kamati kwa kuipongeza serikali kwa kuanza kutekeleza maagizo ya CAG.

Na.Faustine Gimu Galafoni, Dodoma.

 

Leave A Reply