The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Zitto Aachiwa Huru, Apewa Masharti Magumu

0

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Mei 29, 2020 imemuachia huru Zitto Kabwe,  Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, kwa sharti la kutotoa na kuandika maneno ya uchochezi kwa muda wa mwaka mmoja.

 

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Huruma Shaidi, baada ya kumtia hatiani katika makosa yote matatu katika kesi ya uchochezi namba 327/2018.

 

Zitto alikuwa akituhumiwa kwa kutoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki ambapo amekutwa na hatia katika makosa yote matatu ya uchochezi yaliyokuwa yakimkabili.

 

“Naona huko mitandaoni kuna watu wanadai Mahakama ya Kisutu imegeuka kuwa TRA kwa sababu ya faini tunazotoa kwa watuhumiwa. Sasa Zitto mimi nakupa mtoto wa kulea. Sikupigi faini ila nataka usitoe kauli yoyote ya uchochezi katika kipindi cha mwaka mmoja kutoka leo. Mawakili wako watakwambia nini maana ya hukumu hii. Kwa hiyo nakupa wajibu wa kulea amani ya Tanzania kwa kutotoa kauli za kichochezi,” amesema Hakimu Huruma Shaidi.

 

Leave A Reply