The House of Favourite Newspapers

Mbunge Awanyang’anya Wananchi Ambulance kwa Kutompigia Kura Kwenye Uchaguzi

0

Mwanasiasa maarufu nchini Uganda aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo uwaziri, Evelyn Anite Kajik amezua gumzo baada ya kudaiwa kuwanyang’anya gari la kubebea wagonjwa (ambulance), wananchi wa Jimbo la Koboko akiwatuhumu kwamba wameshindwa kumpigia kura na kusababisha akose ubunge.

Evelyn alichaguliwa kuwa Mbunge wa Koboko tangu mwaka 2011 lakini katika uchaguzi wa 2021, aliangushwa na mpinzani wake, Dk. Charles Ayume ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Spika wa Uganda, marehemu Francis Ayume.

 

Kupitia mitandao ya kijamii, Evelyn amewajia juu wanaohoji kwa nini amewapokonya gari hilo wananchi wakati aliwanunulia na kuwakabidhi kipindi akiwa mbunge na kusisitiza kuwa amefanya kitu sahihi.

“Walipokataa kunipigia kura ni kama waliamua kunifukuza, na mimi nikakusanya kila kilichokuwa changu.


“Sasa nasikia wanalia utadhani mimi ndiye niliyeanza kuwakataa. Biblia inasema mshahara wa dhambi ni mauti.

Leave A Reply