The House of Favourite Newspapers

Mbunge Mkuranga Azindua Ulega Cup

1Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega (kulia) akijiandaa kuupiga mpira ili kuzindua mashindano hayo.

2Ulega (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kizomla kabla ya mchezo kuanza.

3Mbunge huyo (katikati kulia)akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Tungi. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Mkamba, Hassan Dunda. 4Akizumgumza jambo na wanamichezo hao kabla ya kuanza kwa mechi hizo.

 

5Ulega (kulia) akiendelea kuzungumza jambo na wanamichezo hao. 6Akiwa katika picha ya pamoja na viongozi, waamuzi na wachezaji.

 

7Akisaini katika kitabu cha wageni baada ya kufika katika hafla hiyo. Anayemshuhudia kushoto ni Diwani wa Kata ya Mkamba. 8Ulega akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kizomla kabla ya mchezo kuanza.

9 Akisalimiana na wachezaji wa timu ya Tungi kabla ya mechi kuanza. 

MBUNGE wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega jana Jumapili alizindua Kombe la Ulega ambalo litavihusiha vijiji vyote vya kata za jimbo hiloambapo mashindano hayo yanatarajiwa kumalizika mwezi Desemba.

10Akifuatilia mechiikiendelea.

Mashindano hayo yaliyoanza katika Kijiji cha Tungi Kata ya Mkamba yanalenga kupatikana kwa timu ya kataitakayowakilisha Mashindano ya Ulega ngazi ya wilaya ambapo timu ya Kizomla ilishinda kwa mabao 3-1 dhjidi ya Tungi kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Shule ya Msingi Tungi.

11Mechi zikiwa zimekwisha kuanza.

Mabao ya washindi yalifungwa na Shaban Abdallah aliyefunga mawili na Hassan Juma huku Rashid Kimoka akifunga kwa upande wa Tungi.

12Mechi kati ya timu ya Tungi na Kizomla zikikipiga uwanjani hapo.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi wa mashindano hayo Ulega alisemaamedhamiria kuinua vipaji vya vijana walio katika wilaya hiyo, kwani anaamini michezo ni burudani pia ni ajira.

13Baadhi ya wananchi waliofika kushuhudia ufunguzi huo.

Akaongeza kuwa wapo vijana wengine wanaweza kuingia katika klabu kubwa zinazoshiriki madaraja mbalimbali ya ligi na hata ligi kuu.

Na Denis Mtima/Gpl

Comments are closed.