The House of Favourite Newspapers

Mbunge Ndumbaro Awaomba Wawekezaji Kuwekeza Jinboni Kwake

0

 

Mbunge wa jimbo la Songea mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk.Damas Ndumbaro amewataka wawekezaji waendelee kuwekeza kwenye jimbo hilo kwa kuwa Serikali ya awamu ya tano imezidi kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo ya umeme.

 

Wito huo ameutoa wakati akifungua Jengo la Kituo cha Redio ya Key Fm lenye thamani ya Sh.Milioni 125 lililopo kata ya Msamala Manispaa ya Songea mkoani humo.

 

Ndumbaro ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema kuwa hakuna sababu ya wawekezaji kushindwa au kuogopa kuwekeza jimboni humo kwa kuhofia miundombinu,maana miundombinu mingi ikiwemo umeme imekamilika.

Akifungua Kituo hicho Ndumbaro amesema kuwa uwekezaji uliofanywa katika ujenzi wa Jengo hilo utawafanya wakazi wa Jimbo hilo pamoja na Majimbo mengine ya mkoa huo kujifunza mambo mbalimbali pamoja na upataji habari ,hivyo ni vema na wadau wengine wakaiga mfano huo.

 

Amesema kuwa licha ya Serikali kuweka miundombinu lakini bado uwekezaji huo utasaidia kupunguza tatizo la Ajira kwa Vijana ambalo limekuwa ni changamoto kwa sasa.

 

“Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk.John Pombe Magufuli imekuwa ikifanya kazi sana hasa katika kuimarisha Miundombinu hapa Nchini ambapo mkoa wa Ruvuma Umeme wa Gridi ya Umeme taifa,Barabara pamoja Uwanja mkubwa wa Ndege “hivyo hakuna sababu ya mwekezaji kuogopa.

 

Kwa upande wake Castory Ndulu ambaye ni mkurugenzi wa Redio hiyo awali akitoa taarifa ya ujenzi wa Jengo hilo la kituo cha Redio amesema kuwa hadi sasa kituo hicho kimetoa Ajira kwa Vijana wapatao 20.

Stori na Amon Mtega toka Songea

Leave A Reply