The House of Favourite Newspapers

Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo Aishauri Serikali Iwekeze Kwenye Kilimo

0
Mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric Shigongo

MBUNGE wa Jimbo la Buchosha Eric Shigongo akitoa hoja Bungeni ameshauri kuwa kama Nchi inataka kurudi kwenye uchumi wa kati basi inatakiwa Serikali na nchi kwa ujumla iwekeze katika kilimo.

 

Amesema Watanzania siyo masikini tatizo ni mfumo ndiyo unafanya Watanzania wawe masikini kwani hawana mazingira wezeshi ya kujikwamua na hali mbaya ya umasikini.

Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba

Shigongo amedai Serikali inatakiwa iiwezeshe TANTRADE ili iweze kufanya utafiti katika masoko kuweza kujua ni kwa aina gani na kwa kiasi gani wakulima walime ili waweze kupata soko la bidhaa zao.

 

Naye Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba wakati akitoa taarifa kwa Mbunge wa Buchosa amedai kuwa Tanzania haijashuka kutoka kwenye ngazi ya uchumi wa kati badala yake ni kipato cha mtu mmoja mmoja ndiyo kimepungua kutoka 7% hadi 4% hivyo haijaathiri pato la Nchi.

Mbunge wa Jimbo la Kawe Josephat Gwajima

“Hatujarudi tulikokuwa, hii naomba isikike vizuri sana hatujawahi rudi uchumi wa chini Nchi yetu bado ipo Middle Income, sasa hivi ambacho kimeathiriwa na Covid na vitu vingine ni Growth Rate tu, (Ukuaji) na yenyewe ni trends zinazobadilika kama mfumuko unavyobadilika.” Alisema Waziri Nchemba.

 

Kwa upande mwingine Mbunge wa Jimbo la Kawe Mchungaji Josephat Gwajima amesema kinachosababisha nchi kushuka kutoka uchumi wa kati ni kutokana na kukosekana kwa dira ya Taifa na maono ya Taifa.

Leave A Reply