The House of Favourite Newspapers

Yanga Yabanwa Mbavu na Tanzania Prisons, Mayele Akosa Penati

0
Kikosi cha Klabu aya Ynaga kilichoanza dhidi ya Tanzania Prisons

KLABU ya Yanga imelazimishwa matokeo ya sare dhidi ya wajelajela Tanzania Prison katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kwenye Uwanja waBenjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

Yanga mabyo licha ya matokeo hayo inaendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu wameongeza alama moja na kufikisha jumla ya alama 57 wakiwaacha wapinzani wao Simba ambao wana alama 46 wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

 

Katika mchezo huo mshambuliaji hatari wa Klabu hiyo raia wa Congo Fiston Mayele alikosa mkwaju wa penati baada ya Feisal Salum kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele amekosa mkwaju wa penati dhidi ya Tanzania Prisons

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kukosa ushindi kwenye mchezo wa 3 mfululizo tangu ipate sare dhidi ya Simba ikalazimishwa sare nyingine dhidi ya Ruvu Shooting na sare ya tatu ni hii ya leo dhidi ya Tanzania Prisons.

 

Prisons wao wanapanda nafasi moja kutoka nafasi ya 15 hadi nafasi ya 14 wakiwa na alama 23, alama moja zaidi ya Ruvu Shooting aliyepokea kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Klabu ya Simba.

Leave A Reply