The House of Favourite Newspapers

Mbunge wa CCM Rukwa Ndyamkama Afariki Hospitali ya Tumbi, Spika Athibitisha

0
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Irene Alex Ndyamkama akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Namkanga wakati wa cha Balozi wa Shina namba 6 ikiwa siku ya pili ya ziara ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa  Julai 8, 2021. (Picha na CCM Makao Makuu)

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt.Tulia Ackson ametangaza kifo cha Irene Alex Ndyamkama ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Aprili 24,2022 na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge jijini Dodoma imeeleza kuwa, Mheshimiwa Ndyamkama amefariki leo Aprili 24,2022 katika Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoani Pwani wakati akipatiwa matibabu.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mheshimiwa Irene Alex Ndyamkama, Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, waheshimiwa wabunge na wananchi wa Mkoa wa Rukwa. Mwenyenzi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,”amesema Mheshimiwa Spika.

 

Aidha, Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Leave A Reply