The House of Favourite Newspapers

RIDHIWAN AMEPOKEA FUTARI KWA JIMBO LA CHALINZE

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete (kushoto)  akipokea msaada wa futari kutoka kwa Arif  Yusuf wa Taasisi ya Dural Irshad Islamic Centre ya Dar es Salaam.
…Akiendelea kupokea misaada.
Sehemu ya misaada iliyotolewa.

 

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete,  amepokea msaada wa futari kutoka kwa taasisi mbili za kidini, kwa ajili ya Waislamu waliopo kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani jimboni humo.

 

Akipokea msaada wa futari hiyo iliyotolewa na taasisi za Dar Irushad Islamia Markaz na Miraj Islamic Centre za jijini Dar es Salaam kwa ajili ya wananchi wasiojiweza, mbunge huyo amesema msaada huo utawafikia walengwa na kuzishukuru taasisi hizo kwa kuwakumbuka wananchi wanaoishi katika mazingira magumu katika mwezi wa Ramadhan.

 

Kwa upande, Arif Yusuf wa taasisi moja miongoni mwa zilizokabidhi misaada hiyo, ameeleza kwamba mwezi huu wa Ramadhan ni wa kumtegemea Mwenyezi Mungu na hivyo wameona ni vyema kula futari na wananchi wasiojiweza wa jimbo la Chalinze lakini akasema kwamba na wao misaada hiyo huipokea kutoka kwa taasisi mbalimbali za nje  ikielekezwa kuwaendea wasiojiweza.

Comments are closed.