The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Mbunge wa Mbozi Aachiwa kwa Dhamana

0
Mbunge Paschal Haonga.

Mbunge wa Mbozi, Paschal Haonga (Chadema) aliyekamatwa na polisi kisha kuwekwa ndani katika Kituo cha Polisi akidaiwa kutoa kauli ya uchochezi ameachiwa kwa dhamana.

 

Inadaiwa Haonga alitoa kauli hiyo hivi karibuni akiwataka wananchi  kwenda kwa mkuu wa mkoa kupinga kauli iliyotolewa na mkuu huyo iliyowataka kutotumia usafiri wa maroli jimboni mwake.

 

Hali hiyo ilisababisha mkuu wa upelelezi wa Mkoa wa Songwe kumweka ndani mbunge huyo kwa saa 48 hadi leo saa 4 asubuhi alipoachiwa kwa dhamana na kutakiwa kurudi kituoni hapo Agosti 18.

Kwa mujibu wa mwansheria wa mbunge huyo amesema polisi bado wanaendelea na upepelezi ili kumfikisha mahakamani.

 

Mkoa wa Songwe ni moja ya mikoa mipya ambayo inakabiliwa na tatizo kubwa la miundombinu mibovu ya barabara, hali ambayo inasabisha usafiri kuwa wa shida.

Wamiliki hushindwa kupeleka vyombo vya usafiri vinavyokubalika kisheria mfano mabasi ambapo wakazi wa Mbozi wanalazimika kutumia usafiri wa malori kutokana na uchache wa mabasi.

NA MOHAMMED ZWNGWA | GLOBAL TV – SONGWE

====

TAZAMA VIDEO AKIFUNGUKA

Leave A Reply