The House of Favourite Newspapers

Mbunge wa Ngorongoro Aachiwa kwa Dhamana, Ashangaa Kukamatwa Bila Kibali Cha Spika – Video

0
Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Ole Shangai akizungumza bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023, jijini Dodoma Juni 22, 2022.

HATIMAYE Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Ole Shangai (CCM) ambaye alidaiwa kushikiliwa na polisi tangu ta Agosti 21, 2023 ameachiwa huru huku akisisitiza kwa kuwa yupo upande wa wananchi lazima apate matatizo, na hilo halitomrudisha nyuma hata siku moja.

Mbunge huyo alidaiwa kushikiliwa na jeshi hilo, akiwa njiani kuelekea kituo cha Polisi wilayani Karatu, kutokana na tuhuma za kuhusishwa kupanga tukio la kushambuliwa waandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 23,  2023 Mbunge huyo amesema amesita kutaja tuhuma alizokutwa nazo na kufafanua kuwa zitajulikana mahakama.

Bila kutaja lini atafikishwa mahakamani, Mbunge huyo wa CCM amedai kwa siku zote tatu alizokuwa ameshikiliwa na polisi hakula chochote.

“Pia nimejifunza kuwa binadamu unaweza kukaa siku tatu bila kula na hautakufa na hata ningekaa siku saba nisingekula siku saba,” amesema.

Aidha, ameeleza kushangazwa na hatua ya polisi kumkamata bila kibali cha Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.

“Ninachoshangaa wote wanajua, polisi ndio wanasimamia sheria zetu na Bunge ndio linatunga sheria niliamini kwamba kama walikuwa wananihitaji na hicho ndio nilikuwa nasubiri wangemuandikia Spika barua alafu Spika anijulishe.

“Nakumbuka mwaka jana Aprili niliitwa kuhojiwa kuhusiana na suala la Loliondo, Spika ndio alitoa kibali cha mimi kuhojiwa nashangaa leo kwanini hawakusubiri mpaka Spika atoe barua… najua kuna presha za kisiasa na mimi ni mwanasiasa nitaendelea kuishi kwenye siasa,” amesema.

Pamoja na mambo mengine amewataka wananchi wajue yeye ni kiongozi wao hata akikamatwa mara 10 ataendelea kuwa na msimamo wao kwa sababu walimchagua kwa ajili yao.

MBUNGE wa NGORONGORO KUKAMATWA -MAWAKILI WAKE WAULIZA – “SPIKA ANA TAARIFA?” -WALIA MATESO ya POLISI

Leave A Reply