The House of Favourite Newspapers

Mbunge wa Simanjiro Ole Sendeka Ashambuliwa kwa Risasi na watu wasiojulikana

0
Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka

MBUNGE wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka ameshambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa ndani ya gari yake.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Lucas Mwakatundu akizungumza amesema tukio hilo limetokea jioni ya Ijumaa Machi 29, 2024.

Amesema limetokea eneo la Ndaleta, wilayani Kiteto wakati Ole Sendeka akiwa na dereva wake akielekea jimboni kwake Simanjiro.

“Ole Sendeka akiwa na dereva wake, gari lao lilishambuliwa kwa risasi ila hawakudhurika ni wazima kabisa,” amesema Kaimu Kamanda Mwakatundu.

Amesema polisi wanaendelea na uchunguzi na hakuna anayeshikiliwa kutokana na tukio hilo.

Leave A Reply